Kiwanda cha kusafisa mafuta cha Dangote huenda kikafikisha kikomo biashara ya mafuta ya miaka mingi kutoka Ulaya hadi Afrika, yenye thamani ya dola bilioni 17 kila mwaka, huku viwanda wa Ulaya vikiwa kwenye hatari ya kufungwa kutokana na ushindani mkubwa uliopo, wachambuzi wanasema.
Mahakama moja ya Tunisia Jumatano imetoa hukumu ya kifo kwa watu wanne, na wengine wawili wamehukumiwa kifungo cha maisha, baada ya kukutwa na hatia ya kumuua mwanasiasa mashuhuri Chokri Belaid miaka 11 iliyopita, yakiwa mauaji ya kwanza ya kisiasa nchini humo ndani ya miongo kadhaa.
Bunge la Togo sasa yakabidhiwa mamlaka ya kumchagua Rais wa nchi hiyo ndogo ya Afrika Magharibi baada ya wabunge kupitisha katiba na kubadilisha mfumo wa nchi hiyo kutoka kwa utawala wa Rais kuelekea mfumo wa bunge.
Maafisa wa usalama wa Kenya Jumanne walianza kutoa miili ya waathiriwa kadhaa wa mauwaji yaliyofanywa na dhehebu lililowataka waumini wao wajiuwe kwa kukaa na njaa ili kwenda kukutana na Yesu
Mgombea wa ushirika wa utawala nchini Senegal, Amadou Ba amempongeza mpinzani wake kutoka kambi ya upinzani Bassirou Diomaye Faye kwa kushinda uchaguzi wa rais, wiki moja baada ya Faye kutoka gerezani.
Jeshi la Nigeria Jumapili liliokoa wanafunzi na wafanyakazi ambao walitekwa nyara na watu wenye silaha kutoka shule moja kaskazini mwa nchi hiyo mapema mwezi huu, jeshi lilisema, siku chache kabla ya tarehe ya mwisho ya kulipa fidia ya $ 690,000.
Papa Francis aliamua katika dakika za mwisho kutokwenda kuhubiri wakati wa Misa ya Jumapili ya matawi katika Uwanja wa St.Peter kuepuka hotuba ndefu mwanzoni mwa wiki takatifu yenye shughuli nyingi ambayo itaipa changamoto afya yake inayozidi kuwa dhaifu.
Upigaji kura ulianza nchini Senegal siku ya Jumapili katika uchaguzi wa rais uliocheleweshwa unaofanyika wakati kuna hali mbaya ya kisiasa ambayo imesababisha maandamano ya kupinga serikali na kuongeza uungwaji mkono kwa upinzani.
Rais Putin ameliita tukio hilo kuwa ni kitendo cha umwagaji damu, cha kikatili na kigaidi na kusema waliohusika moja kwa moja wamekamatwa
Mateka waliookolewa wamekabidhiwa kwa serikali ya jimbo la Sokoto kwa hatua Zaidi, alisema Meja Jenerali Edward Buba.
Jeshi la anga la Ukraine limesema Jumamosi nchi hiyo inaendelea kujikomboa kutokana na mashambulizi ya Russia ya Ijumaa
Vikosi vya Marekani vilifanya mashambulizi ya kujilinda dhidi ya vituo vya kuhifadhi silaha vya chini ya ardhi vya wa-Houthi
Pandisha zaidi