Kimbunga cha tropiki ambacho kimepiga katika kisiwa cha Madagascar wiki hii kimeripotiwa kuuwa takriban watu 18 na kuwakosesha makazi maelfu wengine, ofisi ya dharura ya taifa hilo imesema Ijumaa.
Mtoto wa kiume wa Rais wa Uganda Yoweri Museveni ameahidi kupambana na ufisadi ndani ya jeshi baada ya kuchukua usukani kama kamanda wa juu, hatua inayoonekana kwa kiasi kikubwa kuharakisha hatua ya kuelekea kumrithi baba yake.
Wizara ya Afya ya Ukanda wa Gaza imesema watu zaidi ya 32,000 wameuawa wakati wa mashambulizi ya Israel
China iliweka ushuru kwa mvinyo wa Australia mwaka 2020 wakati wa mzozo wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili
Mivutano ya kisiasa imeongezeka nchini Togo tangu siku ya Jumatatno wakati polisi walipovunja mkutano na wanahabari uliyoitishwa na upinzani ikiwa ni kujibu mageuzi ya kikatiba ambayo yamekosolewa kuwa ni kujitwalia madaraka.
Rais Mahmoud Abbas alimteua Mohammad Mustafa, mshauri wa muda mrefu kuwa Waziri Mkuu wa Palestina mapema mwezi huu.
Chama cha Kejriwal cha Aam Aadmi Party (AAP) kinasema kesi hiyo imetungwa na ina ushawishi wa kisiasa
UN inasema vita vya magenge vimeongezeka wakati wapinzani wenye silaha wakijihusisha na wimbi jipya la mashambulizi
Kiwanda cha kusafisa mafuta cha Dangote huenda kikafikisha kikomo biashara ya mafuta ya miaka mingi kutoka Ulaya hadi Afrika, yenye thamani ya dola bilioni 17 kila mwaka, huku viwanda wa Ulaya vikiwa kwenye hatari ya kufungwa kutokana na ushindani mkubwa uliopo, wachambuzi wanasema.
Mahakama moja ya Tunisia Jumatano imetoa hukumu ya kifo kwa watu wanne, na wengine wawili wamehukumiwa kifungo cha maisha, baada ya kukutwa na hatia ya kumuua mwanasiasa mashuhuri Chokri Belaid miaka 11 iliyopita, yakiwa mauaji ya kwanza ya kisiasa nchini humo ndani ya miongo kadhaa.
Bunge la Togo sasa yakabidhiwa mamlaka ya kumchagua Rais wa nchi hiyo ndogo ya Afrika Magharibi baada ya wabunge kupitisha katiba na kubadilisha mfumo wa nchi hiyo kutoka kwa utawala wa Rais kuelekea mfumo wa bunge.
Maafisa wa usalama wa Kenya Jumanne walianza kutoa miili ya waathiriwa kadhaa wa mauwaji yaliyofanywa na dhehebu lililowataka waumini wao wajiuwe kwa kukaa na njaa ili kwenda kukutana na Yesu
Pandisha zaidi