Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 13:22

Zimbabwe waongoza kwa kuomba hifadhi nje


Watoto wakiokota mahindi yaliyomwagika barabarani wakati wa kusafirishwa kutoka Afrika Kusini kuingia Zimbabwe mwaka jana.
Watoto wakiokota mahindi yaliyomwagika barabarani wakati wa kusafirishwa kutoka Afrika Kusini kuingia Zimbabwe mwaka jana.

Wazimbabwe wanaongoza duniani katika kuomba hifadhi nchi za nje.

Idara ya wakimbizi ya Umoja wa Mataifa - UNHCR - inasema Wazimbabwe wanaongoza duniani katika kuomba hifadhi ya kisiasa katika nchi za nje.

UNHCR inasema Wazimbabwe 158,000 wameomba hifadhi katika nchi za nje mwaka jana, wengi wao katika nchi jirani, Afrika Kusini.

Ripoti hiyo inasema watu kutoka Burma wanashika nafasi ya pili kwa kuomba hifadhi nje. Nchi nyingine ambazo zinatoa waombaji hifadhi nje kwa wingi ni pamoja na Afghanistan, Colombia, Eritrea, Ethiopia na Somalia.

Makadirio yanaonyesha kuwa Wazimbabwe wapatao millioni tatu wamekimbilia Afrika Kusini katika kipindi cha miaka kumi iliyopita kuepuka machafuko ya kisiasa na kutokana na kuanguka kwa uchumi Zimbabwe.

XS
SM
MD
LG