Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 23:39

Zimbabwe yatoa wito wa msaada zaidi kusaidia kukabiliana na ukame


Mkulima wa mahindi akionyesha zao lake mjini Harare.
Mkulima wa mahindi akionyesha zao lake mjini Harare.

Zimbabwe ina takriban watu millioni 2.5 wanaokabiliwa na njaa , na inalaumu mfumo wa hali ya hewa ujulikanoa kama El Nino kwa kusababisha ukame mbaya huko Kusini mwa Afrika

Zimbabwe jumatatu imetoa wito kwa wafadhili wa ndani na wakimataifa kutoa msaada zaidi ikiwa takrian robo ya idadi ya wananchi wake wanakabiliwa na njaa. Umoja wa mataifa unasema serikali ya rais Robert Mugabe lazima iwekeze katika kilimo cha umwagiliaji ili kuzuia upungufu wa chakula.

Zimbabwe ina takriban watu millioni 2.5 wanaokabiliwa na njaa , na inalaumu mfumo wa hali ya hewa ujulikanoa kama El Nino kwa kusababisha ukame mbaya huko Kusini mwa Afrika.

Waziri wa kazi za umma, Saviour Kasukuwere, anasema serikali inatathmini hali ilivyo.

Kasukuwere, alisema, bado tunashughulikia gharama za chakula kinachohitajika, lakini nina hakika tutaweza kukabidhi kwa dunia, kote hapa nyumbani na kimataifa, makadirio tunayotazamia, lakini tunafahamu kuwa baadhi yao tayari wameangukia katika hali ya ukame kwa msimu wa mwka 2016, na tunaamini kuwa idadi hiyo ni takriban watu millioni 2.4, kati ya millioni 26 ambao ndio idadi ya raia wetu walio katika hali ya ukosefu wa usalama wa chakula.

Chimimba David Phiri ni mratibu wa Kusini mwa Afrika katika idara ya chakula ya umoja mataifa FAO. Phiri anasema wanatarajia maafisa wa Zimbabwe kutathmini idadi hiyo kuwa itapanda kwa vile hali ya mfumo wa El Nino itakapokuwa mbaya zaidi. Anasema serikali zinapaswa kuhimiza kilimo cha kuhifadhi ili raia wake wasidhoofishwe na mabadiliko ya hali ya hewa.

Bw. Phiri alisema, tunahiaji kuongeza maeneo ambayo yanafanyiwa kilimo cha umwagiliaji. Kuna vyanzo vingi nchini zimbabawe ambavyo vinatakiwa kufanyiwa ukarabati. Katika nchi za kusini mwa Afrika, Zimbabwe ina idadi kubwa zaidi ya mabwawa, mito na kadhalika, kwa hiyo kuna maji Zimbabwe, pengine zaidi kuliko taifa jengine lolote ambayo yanaweza kutumiwa kama kilimo cha umwagiliaji. Hapo siku za nyuma, hili lilikuwa likifanyika, hamna sababu kwa nini haliwezi kufanyika tena sasa.

Hapo awali Zimbabwe ilijulikana kama mzalishaji mkubwa wa chakula kusini mwa afrika, lakini imekuwa mwagizaji mkubwa wa chakula nje tangu miaka ya elfu mbili. Rais Mugabe analaumu hilo dhidi ya ukame unaotokea mara kwa mara katika kanda hio, lakini wakosoaji wa kiongozi wa Zimbabwe wanasema mradi wenye utata wa mabadiliko ya umiliki wa ardhi, ambao ulilazimisha wakulima wazungu wenye uzoefu kuachia mashamba yao ndio jambo lililo sabisha njaa nchini humo.

XS
SM
MD
LG