Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 09:38

Obama aanzia ziara ya Afrika Senegal


Picha za kwenye mabango za kumkaribisha Rais Obama nchini Senegal, June 24, 2013
Picha za kwenye mabango za kumkaribisha Rais Obama nchini Senegal, June 24, 2013
Rais wa Marekani, Barack Obama na familia yake wanatarajiwa kuwasili mji mkuu wa Senegal, Dakar Jumatano usiku ili kuanza ziara ya wiki moja katika nchi tatu za barani Afrika, ziara ambayo inalenga kuzungumzia kuimarisha taasisi za kidemokrasia na kuchochea uwekezaji wa Marekani barani humo. Rais anasafiri na ujumbe mkubwa wa maafisa wa uchumi wa Marekani, wafanyabiashara na waandishi wa habari.

Rais Obama anaanza ziara yake Alhamisi kwa mazungumzo na Rais wa Senegal, Macky Sall katika makazi ya rais mjini Dakar.

Marais hao wanatarajiwa kujadili masuala ya biashara na wasi wasi wa usalama katika eneo la Sahel barani afrika, ambalo limeona ongezeko la harakati za wanamgambo wa kiislamu.

Uamuzi wa Obama kuitembelea Senegal, taifa dogo la Afrika magharibi ambalo linazungumza lugha ya kifaransa, unaonekana kuunga mkono rekodi na mwenendo wa kidemokrasia za Senegal na juhudi zake za karibuni katika kupambana na rushwa.

Marais Obama na Sall watakuwa na mkutano wa pamoja wa waandishi wa habari kabla ya bwana Obama kuelekea kwenye mahakama kuu ya Senegal ambako atakuwa na maafisa wa sheria wa kieneo.

Wachambuzi wanasema Dakar ni sehemu muafaka kwa mkutano huo. Senegal imefungua mahakama maalum ya Afrika mwaka huu kwa ajili ya kusikiliza kesi ya rais wa zamani wa Chad, Hissene Habre kwa uhalifu dhidi ya binadamu. Itakuwa ni mahakama ya kwanza ya Afrika kusikiliza kesi ya kiongozi wa Afrika katika ardhi ya Afrika.

Rais Obama na familia yake alhamisi mchana watakwenda kisiwa cha Goree, ambacho kilikuwa ni kituo cha mwisho katika biashara ya utumwa kwenye eneo la Atlantic. Kisiwa hicho kimekuwa ni sehemu muhimu kwenda kwa viongozi wa dunia na wamarekani wenye asili ya kiafrika.

Rais na familia yake watatembelea ngome ndogo kisiwani humo inayoitwa nyumba ya watumwa. Unaweza kuingia katika eneo hilo dogo, ambalo halina hewa nzuri ambako watumwa walikuwa wakishikiliwa wakati wakilishwa ili kuhimili safari ndefu kwenye bahari ya altantic.

Rais Obama atahudhuria dhifa ya kitaifa alhamisi usiku na halafu atahitimisha ziara yake nchini Senegal siku ya ijumaa asubuhi kwa mkutano kuhusu usalama wa chakula kabla ya kuelekea nchini Afrika kusini na baadae Tanzania vituo vyake viwili vya ziara yake barani afrika.
XS
SM
MD
LG