Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 20:38

Kerry ayatembelea mataifa ya Ulaya


Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, John Kerry.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, John Kerry.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, John Kerry, ameanza ziara ya siku nne katika nchi za Ulaya leo Jumatatu, ambako atakutana na maafisa kutoka nchi mbali mbali, na kushiriki kwenye mkutano wa viongozi dhidi ya ufisadi.

Mkutano huo wa kupambana na ulaji rushwa utafanyika siku ya Alhamisi chini ya mwenyeji wake, David Cameron, na utahudhuriwa na marais wa Afghanistan, Colombia na Nigeria, kati ya wengine.

Kongamano hilo linakusudiwa kupambana na ufisadi wa kimataifa, na linafanyika siku chache tu baada ya Cameron, kutajwa katika kashfa ya nyaraka za Panama, akisemekana kuwa mdau baada ya baba yake kuwa na akiba ya nchi za nje. Hata hivyo, Waziri huyo mkuu amesema hajafanya kosa lolote. Raia wataweza kuzisoma nyaraka hizo za Panama, ambazo zimewataja viongozi wengi na watu wa ngazi za juu duniani kote, kuanzia leo Jumatatu.

XS
SM
MD
LG