Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 17:52

Marekani yaitaka ZEC ibadili uamuzi wa kufuta uchaguzi Zanzibar


Karatasi za kupiga kura zilizotumika katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 25, 2015
Karatasi za kupiga kura zilizotumika katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 25, 2015

Tume ya uchaguzi ya Zanzibar-ZEC imetakiwa kufikiria kubadili maamuzi yake ya awali ya kufuta uchaguzi wa rais na wawakilishi uliofanyika visiwani humo Oktoba 25 mwaka huu.

Taarifa iliyotolewa na ubalozi wa Marekani nchini Tanzania ilisema imesikitishwa sana na maamuzi haya na kuzitaka pande zote kuonyesha nia ya dhati kwa utaratibu wa demokrasia kwa njia ya amani na uwazi.

Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Zanzibar, bwana Jecha Salim alitangaza kuwa maamuzi ya kufuta uchaguzi wa Zanzibar kwasababu ya dosari kadhaa ambazo zimejitokeza katika zoezi zima la upigaji kura na kuhesabu. Bwana Jecha hakusema uchaguzi mwingine wa visiwa hivyo utafanyika lini.

Mwananchi wa kawaida akipiga kura October 25, 2015.
Mwananchi wa kawaida akipiga kura October 25, 2015.

Taarifa ya ubalozi wa Marekani ilisema inataka tangazo la kufuta uchaguzi na utaratibu wa kutangaza matokeo uendelee na hatimaye kutangazwa mshindi na aliyeshindwa.

Chama cha upinzani cha CUF visiwani Zanzibar kilijibu maamuzi ya ZEC wakisema hawakubaliani na maamuzi hayo. Katibu Mkuu wa CUF ambaye pia ni mgombea urais wa Zanzibar, Maalim seif Sheriff Hamad alisema hatambui maamuzi ya mwenyekiti wa tume kwa vile hakufuata utaratibu wa kufuta uchaguzi wa Zanzibar.

Chama tawala cha CCM ambacho mgombea wake katika nafasi ya Rais wa Zanzibar, Mohammed Ali Shein ambaye pia anawania tena wadhifa huo hajasema lolote kuhusiana na maamuzi haya.

XS
SM
MD
LG