Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 11:59

Zaidi ya watu 300 walibakwa August DRC


Ripoti ya awali kuhusu tukio la ubakaji DRC mwezi August inasema zaidi ya watu 300 walibakwa katika muda wa siku nne.

Ripoti ya awali kuhusu ubakaji uliofanyika mashariki ya DRC mwezi August inasema watu 303 walibakwa na makundi manne tofauti ya waasi katika muda wa siku nne.

Ripoti hiyo iliyotolewa Ijumaa mjini New York inasema wanawake 235, wasichana wadogo 52, wanaume 13 na watoto wa kiume watatu walibakwa katika muda huo wa siku nne. Ripoti inasema wengine walibakwa zaidi ya mara moja.

Msemaji wa Tume ya Haki za Binadamu, Rupert Colville anasema mashambulizi hayo mara nyingi yalikuwa yanatokea mara tu baada ya kiza kuingia. Karibu wapiganaji 200 wa makundi matatu tofauti ya waasi waliingia katika eneo la Walikale wakijifanya wamekuja kuwalinda wanavijiji hao.

Colville anasema waasi hao walishika udhibiti wa kilima muhimu katika eneo hilo na hivyo kukata mawasiliano ya simu. Baada ya hapo "walifunga barabara, na kwa siku nne wakawa wanabaka wanavijiji."

XS
SM
MD
LG