Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 18, 2024 Local time: 16:29

Rais wa Yemen asema hatoruhusu vita vya wenyewe kwa wenyewe


Waandamanaji wanaoipinga serikali ya Yemen wakishikana mikono wakati wa maandamano ya kumtaka Rais Ali Abdullah Saleh ajiuzulu huko Sana'a, May 24, 2011
Waandamanaji wanaoipinga serikali ya Yemen wakishikana mikono wakati wa maandamano ya kumtaka Rais Ali Abdullah Saleh ajiuzulu huko Sana'a, May 24, 2011

Rais wa Yemen Ali Abdullah Saleh akiwa chini ya shinikizo la kimataifa la kujiuzulu anasema hatoiruhusu nchi yake iingia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Bwana Saleh ametoa matamshi hayo Jumatano kukiwa na mapigano makali kati ya majeshi yanayoiunga mkono serikali na wapiganaji wanaomtii kiongozi wa kijadi aliye na nguvu nchini humo, yakiendelea kwa siku ya tatu huko Sana’a. Kiongozi huyo wa kijadi amejiunga na kundi la upinzani linalomtaka Bwana Saleh aondoke madarakani mara moja.

Katika mifululizo ya taarifa na mahojiano na mashirika ya habari, Bwana Saleh pia alisema hatoiruhusu Yemen kuwa taifa lililoshindwa. Aliapa katika mahojiano kadhaa kwamba ataendelea kuwa Rais licha ya maandamano dhidi yake na mapigano ya jeshi la serikali na wapiganaji wa upinzani.

Mapema Jumatano, mashahidi waliripoti kusikia milio mingine ya silaha katika mji mkuu ambapo mapigano kati ya majeshi ya Bwana Saleh na yale yanayomtii mkuu wa kabila la Hashid, Sheikh Sadeq al-Ahmar yamesababisha vifo vya watu wasiopungua 41.

Mashahidi pia wanasema wapiganaji wa mkuu huyo wamechukua udhibiti wa majengo kadhaa ya serikali huko Sana’a. Uamuzi wa Al-Ahmar kuwapeleka wapiganaji wake katika mapigano dhidi ya majeshi ya serikali unaongeza mvutano huko Yemen, takribani miezi minne tangu mgogoro kuzuka.

Siku ya Jumanne Baraza la Ushirikiano la Ghuba, GCC lilitoa wito wa kusitishwa mara maoja mapigano kati ya majeshi ya usalama na wapiganaji wa kikabila.

XS
SM
MD
LG