Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 13:08

Mamilioni ya wayemen wahitaji msaada wa haraka kunusuru maisha yao


Mtoto wa kiume akienda kujaza maji kwa ajili ya matumizi ya nyumbani mjini Sanaa, Yemen, Oktoba 13, 2015.
Mtoto wa kiume akienda kujaza maji kwa ajili ya matumizi ya nyumbani mjini Sanaa, Yemen, Oktoba 13, 2015.

Umoja wa Mataifa umeiomba jumuiya ya kimataifa kuwasaidia mamilioni ya raia katika taifa lililokumbwa na vita la Yemen, ili waweze kujikimu kimaisha huku hali ya kibinadamu nchini humo ikiendelea kuzorota.

Mratibu wa Umoja wa Mataifa kwa Yemen, Jamie Mcgoldrick anaiita Yemen ni mzozo usioonekana, na vita vya huko vimegubikwa na vita ambavyo vinapiganwa nchini Syria. Wakati macho yote yako kwenye matukio yanayojitokeza nchini Syria, anasema hali ya kibinadamu kwa takriban raia milioni 22 wa Yemen inazidi kuwa mbaya sana.

Anasema kiwango cha dharura ni kikubwa mno na kiwango cha mahitaji kimevuka mpaka na kina cha mzozo hakipimiki na maafa ambayo yanaendana na hali hiyo hayasemeki. Kila upande unaogeuka, kila mtu unayekutana naye ameathiriwa na mzozo huu. Kila mtu ambaye unapishana naye katika sehemu yoyote ile nchini humo anauhisi mzozo na anavihisi vita.

Serikali ya Yemen na waasi wa kihouthi wamekuwa katika vita vya wenyewe kwa wenyewe kwa miaka mingi; lakini kina cha uharibifu na kuongezeka kwa hatari kwa jamii ya raia ni kikubwa na kimesambaa tangu Saudi Arabia ilipoanza kampeni za mashambulizi ya anga mwezi Machi mwaka jana.

Mcgoldrick anasema inaonekana kuwa ingawaje mapigano nchini Yemen yamepungua tangu mashauriano ya amani yanayosimamiwa na Umoja wa Mataifa kuanza wiki chache zilizopita. Hata hivyo, anasema hali inaendelea kuzorota kwasababu watu wanashindana na miundo mbinu iliyovurugika nchini humo na kuanguka kwa uchumi. Anasema vita vina athari kubwa sana kwa watoto.

Anasema watoto 10,000 walio na umri wa chini ya miaka mitano wametajwa katika idadi ya watu wazima, lakini ni watoto ambao wamefariki kutokana na maradhi yanayoweza kuzuilika kwasababu ya ukosefu wa huduma, ukosefu wa madawa. Na wanafariki kwa magonjwa kama vile homa ya mapafu na kuharisha. Na vingi ya vifo hivi vinatokana na ukweli kwamba wengi wao wanahusishwa na tatizo la utapiamlo.

Mcgoldrick anasema kiasi cha watu 200,000 wameondoka Yemen, wakati watu milioi mbili na nusu wamelazimika kukimbia makazi yao na waliobaki hawana makazi ndani ya nchi. Mwaka jana Umoja wa Mataifa uliomba kiasi cha dola bilioni 1.8 kuwapatia msaada takriban wayemen milioni 7.6 ambao wakati katika mazingira hatari. Bahati mbaya ni asilimia 17 tu ya msaada uliombwa ndiyo umepokelewa.

XS
SM
MD
LG