Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 09:21

Kesi ya Ruto, Sang yaingia awamu muhimu ICC


Naibu wa Rais wa Kenya, William Ruto, anaonekana hapa akisalimiana na wakili wake Karim Khan, mjini The Hague, Uholanzi kabla ya kuhudhuria moja ya vikao cha mahakama ya ICC.
Naibu wa Rais wa Kenya, William Ruto, anaonekana hapa akisalimiana na wakili wake Karim Khan, mjini The Hague, Uholanzi kabla ya kuhudhuria moja ya vikao cha mahakama ya ICC.

Na BMJ Muriithi

Kesi inayomkabili naibu wa rais wa Kenya katika Mahakama ya kimataifa ya ICC mjini The Hague, Uholanzi, iliingia mkondo muhimu siku ya Jumanne wakati majaji wa mahakama hiyo walipoanza kusikiliza hoja ambayo imewasilishwa na mawakili wa Bw. William Ruto wakitaka kutupiliwa mbali kwa kesi hiyo.

Waendesha mashitaka mapema Jumanne walijaribu kushawishi majaji kutofuta mashitaka ya uhalifu dhidi ya ubinadamu yanayomkabili Ruto kwa shutuma za kushiriki katika ghasia za baada ya uchaguzi kati yam waka 2007 na 2008.

Kusikilizwa kwa mara ya kwanza kwa hoja hiyo katika majengo mapya ya mahakama hiyo iliyopo The Hague, kulifunguliwa na mwendesha mashitaka Antony Steynberg kwa kuwaeleza majaji watatu kwamba ana ushahidi wa kutosha wa kumtia hatiani Makamu wa Rais Ruto.

Upande wa mashitaka unashikilia kwamba Ruto na mwanahabari Joshua Sang wana kesi ya kujibu, na kuitaka mahakama hiyo kukubali ushahidi uliobatilishwa.

Lakini Kiongozi wa mawakili wanaomwakilisha Ruto, Karim Khan, ameiambia mahakama hiyo kwamba Ruto na Sang hawana kesi ya kujibu kwani “Bensouda hakuweza kuwasilisha ushahidi wa kutosha kuwa washitakiwa hao walitekeleza mauaji na vurugu zilizotokea kufuatia uchaguzi mkuu huko nchini Kenya."

Kusikizwa kwa hoja hiyo kulirejerewa baada ya kulihairishwa mwezi Novemba mwaka jana, wakati Ruto aliiomba mahakama kufanya hivyo, ili kumpa nafasi ya kuwepo nchini Kenya wakati wa ziara wa kiongozi kanisa la Katolilki duniani, Papa Francis.

Ruto aliwasili Uholanzi siku ya Jumatatu, akiwa ameandamana na mkewe, Rachael Ruto, na wanasiasa kadhaa, wakiwemo maseneta na wabunge ambao waliongozwa na viongozi wa shughuli za seneti na bunge la taifa, Kithure Kindiki na mwenzake Aden Duale.

Akizungumza na Sauti ya Amerika kwa njia ya simu kutoka The hague siku ya Jumanne, Seneta anayewakilisha Kaunti ya Embu, Lenny Kivuti, alisema ana matarajio makubwa kwamba washitakiwa hao wawili wataachiliwa huru. "Nimesikiliza kwa makini yale upande wa mashitaka umeiambia mahakama hivi leo. Wanataka ushahidi uliobatilishwa utumiwe, na hicho ni kinyume cha sheria hata katika mahakama nyingine yoyote ile ulimwenguni. Nina hakika hata majaji wameona kwamba upande wa mashtaka unang'ang'ana tu bila ushahidi wa kutosha. Sioni Ruto na Sang wakipatikana na hatia kwani hawana kesi ya kujibu," alisema Kivuti Jumanne jioni.

Lakini wakili Agina Ojwang ameiambia sauti ya Amerika kutoka Nairobi kwamba endapo wawili hao watapatikana na kesi ya kujibu na hatimaye kuhukumiwa, basi litakuwa ni funzo kwa wengi barani Afrika ambao alisema wamekuwa wakivunja sheria na kuwakadamiza wananchi bila kujali. Sikiliza mahojiano hayo:

please wait

No media source currently available

0:00 0:07:27 0:00
Kiungo cha moja kwa moja


XS
SM
MD
LG