Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 18:37

WHO yaeleza kuwa hewa chafu yazidi kuathiri dunia


Hali ya ukungu ulotanda huko Shanghai , China
Hali ya ukungu ulotanda huko Shanghai , China
please wait

No media source currently available

0:00 0:02:18 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Utafiti umegundua kwamba zaidi ya aslimia 80 ya watu wanaoishi mijini wanaathiriwa na viwango vikubwa vinyavotisha vya hali chafu ya hewa, inayowajibika kwa vifo vya mapema millioni 7 kila mwaka. Ripoti hii mpya juu ya hali ya hewa iliyofanywa na shirika la afya duniani imeeleza kuwa wengi wa wale walioaathirika wanaishi katika miji mikuu maskazini zaidi duniani.

Inaeleza kuwa asli mia 98 ya miji katika nchi zilizo maskini zaidi na zenye wakazi takriban laki moja wanaathiriwa na viwango vikubwa zaidi vya hewa chafu kuliko inavyopendekezwa na shirika la WHO. Idadi hiyo inapungua hadi asli mia 56 katika nchi tajiri.

WHO inaonya kwamba kushuka kwa ubora wa hali ya hewa katika maeneo ya mijini inazidisha athari za kupata magonjwa ya kupooza, magonjwa ya moyo, saratani ya mapafu, na magonjwa sugu katiika mfumo wa kupumua, kama vile pumu. Lakini mkurugenzi wa WHO katika masuala ya afya ya umma na sera za mazingira, Bi Maria Neira, anasema hatua bora zaidi zinaweza kuchukuliwa kuboresha hewa na hivyo kuzuia magonjwa na vifo.

Bi Neira anasema, utaona kuwa katika miji ambapo hatua zimechukuliwa, unaona kupungua viwango vya hewa chafu na hivyo hatari za kiafya zinazosababisha na hewa chafu pia inapungua.

Taarifa katika Utafiti huo umeeleza kuwa vifo vinavyosababishwa na uchafu wa hewa vinaweza kupunguzwa kwa asilimia 15 .

Mratibu wa idara ya afya ya umma na sera za magingira katika shirika la WHO Carlos Dora, anasema hata katika miji masikini hewa inaweza kuboreshwa kwa kuongeza mikakati yenye gharama nafuu ikiwa ni pamoja na utumiaji wa nishati mbadala kama vile upepo na jua na mfumo enedelevu ya usafiri wa umma.

Bw Dora anasema, iwapo una mfumo msafi wa usafiri kama vile kuendesha baiskeli au usafiri wa haraka, Ambapo una watu wengi wanaosafirishwa kwa kutumia magari kidogo, basi utakuwa na hali ndogo ya uchafu wa hewa . Au katika miji kama vile New York ambao kwa kiasi kikubwa umesafisha mafuta yanayotumiwa kutia joto au baridi majengo , basi utakuwa na maendeleo muhimu katika kusafisha hewa.

Ripoti inasema miji ambayo ina hewa chafu ipo maeneo ya mashariki ya Mediterennean na kusini mashariki mwa Asia ikifwatiwa na Afrika.

XS
SM
MD
LG