Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 15:38

Utoaji habari White House Wakera Waandishi


Waandishi wanaondoka baada ya mkutano huo kumalizika chini ya utaratibu mpya wa upashaji habari White House.
Waandishi wanaondoka baada ya mkutano huo kumalizika chini ya utaratibu mpya wa upashaji habari White House.

White House imekosolewa vikali siku ya Ijumaa baada ya kuzuia baadhi ya vyombo vya habari kuhudhuria utaratibu uliyopo wa kila siku wa maswali na majibu yanayofanywa na Msemaji wake Sean Spicer.

Baadhi ya vyombo vya habari ambavyo vimekuwa vikimkosoa Rais Donald Trump, ikiwemo CNN na New York Times ni kati ya vile vilivyozuiliwa kuhudhuria utaratibu huo wa kupashwa habari.

Lakini vile vyombo vya habari ambavyo vinaonekana kutomkosoa Trump, vikiwemo; kituo cha habari Breitbart News, mtandao wa habari wa “The One America News Network” na gazeti la “Washington Times” viliruhusiwa kuhudhuria au walikaribishwa katika utaratibu wa maswali na majibu Ikulu ya Marekani.

Vyombo vya habari vingine maarufu kama vile “ABC”, “CBS”, “NBC” na kituo cha Fox broadcast networks viliruhusiwa.

Hata hivyo vituo vingine, likiwemo shirika la habari la “The Associated Press,” kwa kuonesha mshikamano na vituo vilivyo zuiliwa kuhudhuria utaratibu wa kila siku wa kupata habari huko White House, vilikataa kuhudhuria.

Mwandishi wa habari wa VOA anayefuatilia habari za White House Ijumaa alikuwa hajakaribishwa kuhudhuria utaratibu wa kupashwa habari na hivyo hakuweza kuingia kwenye mkutano huo na Spicer.

Mkutano na Spicer ulikuwa bila ya kamera—ambao waandishi wanaoripoti White House wanauita ni “gaggle” neno lenye maana ya sio rasmi,-- ulifanyika katika ofisi ya Spicer badala ya kufanyika katika chumba cha habari, ambapo ni mahali rasmi kwa shughuli za kupata habari, na waandishi wote walio na vibali wanahaki ya kuhudhuria.

Chama cha Wanahabari wanaoripoti habari za rais White House, wamelalamika kuwa kitendo cha White House kubadilisha utaratibu na watalizungumzia hilo zaidi.

“Chama cha waandishi kimepinga vikali namna ambavyo utoaji habari usio rasmi unavyo endeshwa na White House,” amesema Jeff Mason, Kiongozi wa Umoja huo ambaye anafanya kazi na shirika la habari la Reuters.

Naibu msemaji wa White House Sarah Huckabee Sanders alitetea kuwa utaratibu wa maandalizi ya kutoa habari Ijumaa ulitayarishwa kwa mujibu wa utaratibu ule ule ulio na viwango unaotumika White House.

“Tunajaribu kufanya mikutano ambayo sio rasmi,” ameiambia VOA kwa simu. “Tulikuwa na waandishi walioruhusiwa kuhudhuria mkutano na kila mmoja amewakilisha na kupata habari. Na kulikuwa na nafasi ya ziada kidogo kwenye ofisi ya Spicer, kwa hiyo waandishi wengine wachache waliruhusiwa.”

XS
SM
MD
LG