Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 23, 2024 Local time: 13:36

Waziri wa zamani wa Misri ahukumiwa kifungo cha jela


Waziri wa zamani wa Misri ahukumiwa kifungo cha jela
Waziri wa zamani wa Misri ahukumiwa kifungo cha jela

Waziri wa zamani wa utalii ahukumiwa kifungo cha miaka mitano jela kwa tuhuma za rushwa.

Mahakama moja nchini Misri imehukumu waziri wa zamani wa utalii kifungo cha miaka mitano jela kwa tuhuma za rushwa.

Vyanzo vya kisheria vinasema kuwa mahakama ya Cairo imemkuta na hatia Zuheir Garana leo Jumanne kwa makusudi kutumia vibaya fedha za umma na kuwaruhusu wafanyabiashara wawili kununua ardhi ya taifa kinyume cha sheria. Wafanyabiashara hao pia walihukumiwa adhabu ya kifungo.

Garana ni waziri wa pili mwandamizi katika serikali ya rais wa zamani Hosni Mubaraka kukutwa na hatia ya rushwa kufuatia ghasia dhidi ya serikali ambazo zilipelekea Bwana Mubarak kujiuzulu wadhifa wake mwezi February.

Wiki iliyopita mahakama nyingine ya Misri ilimhukumu waziri wa zamani wa mambo ya ndani, Habib el-Adly kifungo cha miaka 12 jela. Mahakama hiyo pia ilimtoza el-Adly faini ya dola milioni mbili na nusu kwa makosa ya rushwa, ikiwa ni pamoja na kufanya biashara haramu ya mzunguko wa fedha. Hivi sasa anakabiliwa na makosa tofauti yanayohusu mauaji ya waandamanaji waliokuwa wanaunga mkono demokrasia, hii ni kwasababu alikuwa ni mkuu wa majeshi ya usalama.

Waendesha mashtaka pia wameanzisha uchunguzi kuhusu rushwa na matumizi mabaya ya madaraka dhidi ya rais wa zamani na watoto wake wawili wa kiume, Gamal na Alaa.

XS
SM
MD
LG