Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 18, 2024 Local time: 15:20

Waziri Mkuu mteule wa Italy kuunda serikali mpya


Waziri mkuu mteule wa Italy Mario Monti.
Waziri mkuu mteule wa Italy Mario Monti.

Mario Monti asema atafanya kila juhudi kufufua uchumi na kujenga upya fahari ya Italy.

Waziri mkuu mteule nchini Italy Mario Monti ambaye zamani alikuwa kamishina katika Jumuiya ya Ulaya, ameombwa na rais nchini humo kuunda serikali mpya. Hatua hiyo imetangazwa siku moja baada ya Waziri Mkuu Silvio Berlusconi kujiuzulu kufuatia wasiwasi wa jamii ya kimataifa juu ya mzozo wa kifedha huko Italy. Baada ya mikutano 17 na wanasiasa wa ngazi za juu Jumapili rais wa Italy Giorgio Napolitano alimwomba Mario Monti kuunda serikali mpya. Kamishina huyo wa zamani wa Jumuiya ya Ulaya anasema atafanya kila juhudi kufufua uchumi na kujenga upya fahari ya Italy. Washirika wa zamani katika serikali ya mseto wamekataa kumuunga mkono bwana Monti kama Waziri Mkuu, na badala yake wanapendekeza kuitishwe uchaguzi wa mapema. Wachambuzi wanasema hii ni ishara kuwa Waziri Mkuu mpya mteule anakabiliwa na changamoto kuu kuweza kutekeleza hatua zilizoidhinishiwa na bunge wiki jana kupunguza deni kubwa la umma nchini humo. Kuteuliwa kwa Mario Monti kama Waziri Mkuu mpya wa Italy kulitangazwa chini ya siku moja baada ya Silvio Berlusconi kujiuzulu ambapo watu walisherehekea sana katika barabara za mji mkuu wa Roma. Mikopo ya Italy iliongezeka wiki jana na wawekezaji wakasema bayana kuwa wanamtaka Berlusconi ajiuzulu. Alihutubia taifa kwa njia ya Televisheni Jumapili.

XS
SM
MD
LG