Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 15:55

Watu watano wauwawa, waangalizi watembelea miji muhimu


Devrilmiş prezident Məhəmməd Mursini dəstəkləyənlər Qahirə universitetinin qarşısında toplaşıb - 16 iyul, 2013<br />
<br />
Devrilmiş prezident Məhəmməd Mursini dəstəkləyənlər Qahirə universitetinin qarşısında toplaşıb - 16 iyul, 2013<br /> <br />

Watu watano wauwawa wakati waangalizi wakijiandaa kutembelea maeneo ya Daraa, Hama na Idlib yalioathirika zaidim na ukandamizaji huo.

Mashirika ya haki za binadamu yamesema majeshi ya Syria yameuwa watu watano leo wakati waangalizi wa Umoja wa nchi za kiarabu Arab League wakielekea kwenye miji mitatu muhimu ambako serikali imekuwa ikikandamiza upinzani.

Wanaharakati wanasema baadhi ya vifo vya alhamisi vilitokea karibu na Damascus baada ya majeshi ya usalama kufyatua risasi kwa waandamanaji wanaoipinga serikali.

Ghasia hizo zilitokea wakati waangalizi wakijiandaa kutembelea maeneo ya Daraa, Hama na Idlib kufuatilia ahadi za serikali kusimamisha ukandamizaji mkali na kuwaachia wafungwa wa kisiasa.

XS
SM
MD
LG