Polisi kusini mwa Nigeria wanasema washambuliaji wamerusha bomu kwenye shule ya kiarabu huko kusini, na kujeruhi watu 7 siku kadhaa baada ya mfululizo wa mabomu yaliouwa watu katika makanisa nchini humo.
Maafisa wanasema mlipuko huo ulitokea Jumanne katika jimbo la Delta wakati bomu hilo la kutengenezwa kienyeji lilirushwa kutoka kwenye gari. Watoto 6 ni kati ya waliojeruhiwa.
Shambulizi hilo linafuatia mfululizo wa mabomu manne yaliouwa watu wapatao 39.