Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 12:56

Watu 60 wafariki Ivory Coast


Baadhi ya nguo na viatu vya waliofariki katika mkanyagano mjini Abidjan, January 1, 2013.
Baadhi ya nguo na viatu vya waliofariki katika mkanyagano mjini Abidjan, January 1, 2013.
Maafisa wa serikali nchini Ivory Coast wanasema takriban watu 60 wamefariki wakati wa mkanyagano wa sherehe za mwaka mpya mjini Abidjan. Wengine 50 walijeruhiwa katika mkasa huo ambao ulitokea mapema Jumanne katika wilaya ya Plateau kwenye uwanja wa mpira ambapo watu walikusanyika kujionea fataki zikirushwa kuukaribisha mwaka mpya. Televisheni ya AIP nchini Ivory Coast inaripoti kwamba wengi wa waathirika walikuwa vijana. Wazazi wakiwa na huzuni walikwenda kwenye uwanja wa mpira wakiwatafuta watoto wao. Haikufahamika mara moja ni nini kilikuwa chanzo cha mkanyagano huo.
XS
SM
MD
LG