Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 01:34

Watu 40 wauawa Yemen


Rais wa Yemen Abdullah Saleh
Rais wa Yemen Abdullah Saleh

Mapigano yanaendelea katika mji mkuu wa Yeman wa Sanaa, kati ya wapiganaji wa upinzani na wanajeshi wa serikali. Mauaji yaongezeka Yemen siku moja baada ya rais Saleh kurejea

Mapigano baina ya makundi yanayounga mkono serikali ya Yemeni na yale yanayoipinga yamesababisha vifo vya watu 40 Jumamosi siku moja tu baada ya rais Abdallah Saleh kurejea nchini humo bila kutarajiwa na kutoa mwito wa kusitishwa mapigano.

Mapigano ya Jumamosi yalizuka katika mji mkuu Sana’a ambapo majeshi ya serikali yamekuwa yakipambana na wapinzani wake.Wanaharakati wanasema majeshi ya serikali yalipigana na makundi yanayounga mkono mashehe wa kikabila ambao hawamuungi mkono tena rais Saleh.

Wanasema pia kuwa majeshi hayo yamewafyatulia risasi waandamanaji waliokuwa wamepiga kambi katika kambi inayojulikana kama Change Square. Bwana Saleh alitoa mwito wa kuhitimishwa kwa ghasia mara tu aliporejea Yemen Ijumaa kutoka Saudi Arabia.

Alikuwa nchini Saudi Arabia kwa miezi mitatu akitibiwa kufuatia majeraha aliyopata mwezi Juni baada ya shambulizi katika makao ya rais mjini Sana’a. Katika taarifa rais huyo alisema suluhu la mgogoro dhidi ya serikali yake ni majadiliano na wala sio matumizi ya bunduki.

XS
SM
MD
LG