Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 16:41

Watu 150 waandamana Kabul kupinga mauaji ya mwanamke

Askari akiwa katika harakati za kutuliza Ghasia Kabul
Askari akiwa katika harakati za kutuliza Ghasia Kabul

Watu walioshiriki katika maandamano ya jumatano mjini Kabul wakiwemo wanawake wa kutetea haki za binadamu wamedai waliohusika kufikishwa katika mkondo wa sheria.

Takriban watu 150 wameandamana Jumatano katika mji wa Kabul kupinga mauaji ya mwanamke yalirekodiwa katika video.

Picha ambayo zilipatikana na vyombo vya habari na kusambazwa katika mtandao wa internet inaonesha picha ya mwanamke katika jimbo la Parwan akiwa amepigwa risasi hadi kufa . Maafisa wa ndani wanasema Taliban wanamshutumu mwanamke kwa kufanya vitendo vya uzinifu ambavyo ilipelekea kuhukumiwa mwezi uliopita.

Rais wa Afghanistan Hamid Karzai , umoja wa mataifa na kamanda wa Marekani na majeshi ya NATO nchini Afghanistan Generali John Allen wote wameshutumu vikali mauaji hayo.

Watu walioshiriki katika maandamano ya jumatano mjini Kabul wakiwemo wanawake wa kutetea haki za binadamu wamedai waliohusika kufikishwa katika mkondo wa sheria.

Wakati wa utawala wa Taliban nchini Afghanistan katika miaka ya 1990 wanawake walipigwa marufuku kufanya kazi , kupata elimu au kuacha nyumba zao bila kusindikizwa na mwanaume.

XS
SM
MD
LG