Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 08:04

Watano wauwawa nchini Mali


Picha ya Maktaba: Wanamgambo wa moja ya vikundi vya kislam huko Mali.
Picha ya Maktaba: Wanamgambo wa moja ya vikundi vya kislam huko Mali.

Watu watano wameuwawa baada ya watu wenye bunduki wanaoaminika kuwa wapiganaji wa Al-Qaida kushambulia kituo cha kijeshi kilichoko katikati ya Mali.

Tukio hilo limefanyika usiku wa kuamkia Jumatatu kwenye mji wa Nampala ulioko kilomita 530 kaskazini mwa mji mku wa Mali, Bamako, karibu na mpaka wa Mauritania.

Afisa mmoja kutoka Nampala ameiambia Sauti ya America (VOA) kwamba wanajeshi watatu wa Mali, pamoja na wapiganaji wawili wameuwawa kwenye mapigano hayo.

Hakuna aliyetangaza kuhusika na mauaji hayo lakini kundi la Al-Qaida, linashukiwa kuhusika na limekita mizizi katika eneo hilo.

Kundi la Al Qaida lililoko ukanda wa Islamic Magreb, pamoja na vikundi vingine vilijtwalia sehemu kubwa ya kaskazini mwa Mali, mwaka 2012 kabla ya kuondolewa na wanajeshi walokuwa wakiongozwa na Ufaransa.

XS
SM
MD
LG