Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 17:50

Wanyarwanda wapiga kura kumchagua rais


Kampeni za uchaguzi wa rais Rwanda
Kampeni za uchaguzi wa rais Rwanda

Wapiga kura wa Rwanda wanapiga kura hii leo kumchagua kiongozi mpya kwa mhula mwengine wa miaka saba. Rais Paul Kagame yuko tayari kuondoka asipochaguliwa.

Wagombea kiti cha rais huko Rwanda walimaliza kampeni zao mwishoni mwa wiki, wakati nchi hiyo inajiandaa kwa uchaguzi Juamtatu. Licha ya changa moto kutoka kwa viongozi watatu wa upinzani, rais Paul Kagame anatarajiwa kurudishwa madarakani.

Rais wa Rwanda Paul Kagame, alimaliza kampeni yake ya kuwania kiti cha rais kwa mara ya pili, mbele ya wafuasi elfu 50, nje kidogo ya mji mkuu Kigali. Wakati wa mkutano huo, hotuba za kumuunga mkono rais Kagame zilishindikizwa kwa nyimbo na shangwe zinosifu uwongozi wake. Waimbaji mashuhuri wa Rwanda pia waliimba kwenye hafla hiyo.

Akisimama mbele ya umati wa watu akiwa amevaa vazi lenye rangi nyekundu, nyeupe na blue ambazo ni rangi za chama cha Rwanda Patriotic Front, Bw. Kagame aliwashukuru watu kwa usaidizi wao wakati wa kampeni, akisema anamipango mikubwa kwa taifa hilo la afrika ya kati.

Wakati huo huo huko Kigali, mkutano wa mwisho wa chama cha Social Democratic Party cha mgombea Jean Damascene Ntawukuriryayo, haukuwa na tamasha nyingi. Akisimama mbele ya wafuasi elfu kadhaa, Bw. Ntawukiriryo aliwaomba wanyarwanda kumpa kura zao. Mwakilishi wa PSD pengine ndiye pekee anaewakilisha change moto kubwa zaidi kwa bw. Kagame, lakini hatarajiwi kumtia wasiwasi bw Kagame ambaye alichaguliwa mwaka 2003 kwa asli mia 95 ya kura.

Changa moto kutoka kwa wagombea Prospero Higiro na Alvera Mkabaramba, pia haziusababisha mshtuko wowote. Wafatiliaji wanasema mipango ya maendeleo ambayo vyama vya upinzani vinapendekeza ni takriban sawa na ile ya chama cha RPF. Hapo mwaka 2003, vyama hivyo vitatu vilimuunga mkono Bw. Kagame katika uchaguzi wa kwanza tangu mauwaji ya halaiki, na wakosoaji wamewataja kama ni vibaraka wa chama tawala, ili kuonyesha tu kuna upinzani kwenye uchaguzi huo.

Japo Bw Kagame anaonekana anaungaji mkono wa kila mtu, lakini wafwatiliaji wengi wakimatiafa wanasema serikali yake imekandamiza upinzani wa kweli.
Hapo mwezi Aprili mgombea mpinzani Vitoire Ingabire, alikamatwa na serikali ya Rwanda na kushtakiwa kwa makosa ya kukanaa mauwaji ya halaiki. Ingabire alirejea kutoka uhamishoni mapema mwaka huu ili kuandaa kampeni yake ya uchaguzi lakini hakuweza kujisajili kwa uchaguzi huo.

Tuhuma nyengine ya hivi karibuni ni kuwa vikosi vya usalama vya Rwanda vinashukiwa kuhusika katika jaribio la kumuuwa jenerali Faustin Nyamaswa huko Afrika kusini, akiwa uhamishoni. Rwanda ilikanusha mashtaka hayo, lakini Afrika kusini ilimuita balozi wake nyumbani kwa malalamiko.

XS
SM
MD
LG