Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 03:11

Wanawake Sudan Kusini waomba kupatiwa nafasi za uongozi


Sarah Rial anasema wakati umefika kwa wanawake kushirikishwa kwenye uongozi Sudan Kusini.
Sarah Rial anasema wakati umefika kwa wanawake kushirikishwa kwenye uongozi Sudan Kusini.

Wanaharakati wa haki za wanawake nchini Sudan Kusini wanatoa wito kwa viongozi wa serikali ya mpito ya umoja wa kitaifa kuwajumuisha wanawake zaidi katika idara tofauti za serikali ambazo zinatarajiwa kuundwa.

Wanawake hao walitoa wito wao Jumatano mwanzoni mwa mkutano wa kitaifa wa siku mbili mjini Juba. Zeinab Yassin, mwenyekiti wa muungano wa chama cha wanawake wa Sudan Kusini alisema mkutano huo ni muhimu kwa wanaume na wanawake kuelimishana juu ya kile kilichojumuishwa katika mkataba wa amani uliotiwa saini na Rais Salva Kiir na Makamu wa kwanza wa Rais, Riek Machar, kiongozi wa zamani wa uasi.

Bibi Yassin alisema wanawake wa Sudan Kusini lazima wafahamu kile kilichomo katika mkataba wa amani kabla ya kuzungumza kuhusu jukumu la wanawake katika utaratibu wa maridhiano na uponyaji.

Alitoa wito kwa viongozi wa Sudan Kusini kuwajumuisha wanawake katika tume ya ukweli, maridhiano na uponyaji ambayo bado haijaundwa.

XS
SM
MD
LG