Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 08:21

Wanaoishi na HIV Kenya wanawataka viongozi kutekeleza ahadi zao


Mwanamke mwenye virusi vya HIV akijitayrisha kula dawa kupambana na ugonjwa huo hatar.
Mwanamke mwenye virusi vya HIV akijitayrisha kula dawa kupambana na ugonjwa huo hatar.

Mkutano wa kwanza wa kitaifa juu ya ukimwi Kenya ulifunguliwa Nairobi, kukiwepo na wito wa kutekelezwa ahadi za kugharimia vita dhidi ya HIV/Ukimwi

Mkutano wa kwanza wa Kitaifa juu ya Ukimwi ulifunguliwa rasmi Jumatano mjini Nairobi na waziri wa mipango maalum Bi. Esther Murugi, lakini uligubikwa na makelele kutoka kwa kundi la watu wanaoishi na HIV.

Kundi hilo la mamia ya watu liliwasili kwenye ukumbi wa mkutano baada ya kuandamana kwenye njia za Nairobi, wakiimba na kutoa makaula kama vile, "Mlitoa ahadi! wakati umefika kutekeleza" na "Munazungumza na sisi tunafarik!"

Maandamano yalipangwa na mwakilishi wa shirika la afya la Kimarekani GAP nchini Kenya Paul Davis, anaeleza kwamba "Hii leo watu 350 wanaoishi na HIV na wanaowaunga mkono kutoka kila pembe ya nchi, wamekuja katika sherehe za ufunguzi wa mkutano wa Taifa juu ya Ukimwi ili kuwaomba viongozi kutekeleza ahadi zao za kugharimia kwa kikamilifu vita dhidi ya HIV/Ukimwi."

Ingawa makauli ya waandamanaji yalimshambulia zaidi waziri Murugi, lakini maandamano yalilengwa zaidi dhidi ya rais Barack Obama na waziri wa fedha wa Kenya Uhuru Kenyatta kwa kutotekeleza ahadi zao walizotowa awali.

XS
SM
MD
LG