Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 12:22

Wananchi wa Kenya wahofia kuzuka ghasia katika uchaguzi mkuu ujao


viongozi wa kisiasa nchini kenya wakiwa kwenye mkutano na wananchi
viongozi wa kisiasa nchini kenya wakiwa kwenye mkutano na wananchi

viongozi na wanasiasa warushiana maneno makali kwenye majukwaa ya kisiasa nchini Kenya.

Ikiwa imesalia mwaka mmoja tu kabla ya uchaguzi mkuu wa rais na bunge nchini Kenya, viongozi na wanaiasa wameanza kurushiana maneno makali kwenye majukwaa ya kisiasa nchini Kenya.

Ingawa serikali ya Kenya imeunda taasisi maalumu ya kuwafikisha mahakamani wanasiasa wanaoeneza chuki na uchochezi wa kikabila mpaka sasa hakuna kiongozi wa kisiasa aliyehukumiwa mahakamani kwa hotuba hizo za chuki.

Hali hiyo imepelekea wasiwasi kwa wananchi wa Kenya , wakihofia uwezekano wa kuzuka tena ghasia na machafuko ya kisiasa kama ilivyofanyika katika uchaguzi mkuu uliopita.

Wanasiasa waohusika zaidi na hotuba hizi za uchochezi ni pamoja na waziri mkuu raila odinga, naibu waziri mkuu uhuru kenyata na aliyekuwa zamani waziri wa elimu ya juu William Rutto ambaye ni kigogo wa kisiasa katika jimbo la Rift Valley.

Na kutokana na chuki na uhasama huu wa kisiasa rais Mwai Kibaki wa Kenya aewataka viongozi hawa kukomesha hotuba za chuki na uchochezi kati yao.

XS
SM
MD
LG