Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 06:26

Wanajeshi zaidi kupelekwa Mali


Mwanajeshi katika kituo cha ukaguzi cha Diabaly nchini Mali, January 21, 2013.
Mwanajeshi katika kituo cha ukaguzi cha Diabaly nchini Mali, January 21, 2013.
Maafisa wa Umoja wa Mataifa wanasema kikosi cha kuingilia kati cha Afrika kilichopelekwa Mali kinaweza kuongezwa kwa mara mbili ya idadi ya hivi sasa na kufikia takribani wanajeshi 3,300 iwapo wanajeshi zaidi wanahitajika ili kuchukua udhibiti kutoka kwa wanamgambo wa ki-Islam wanaoshikilia upande wa kaskazini mwa nchi hiyo.

Balozi wa Ivory Coast katika Umoja wa Mataifa, Youssoufou Bamba ambaye anaiwakilisha Jumuiya ya kiuchumi ya nchi za Afrika Magharibi-ECOWAS kwenye Umoja wa Mataifa anasema takribani wanajeshi 1,000 tayari wapo Mali. Alilisihi Baraza la Usalama Jumanne kutoa msaada wa dharura wa fedha na vifaa kwa operesheni hiyo.

Majeshi ya Ufaransa na Mali yamefanikiwa kuwazuia wanaharakati waliochukua udhibiti wa sehemu kubwa za kaskazini ya Mali kuelekea upande wa kusini.

Balozi wa Mali aliwashukuru wanachama wa Baraza la Usalama pamoja na wale waliotoa msaada na wanajeshi ili kupigana na wanamgambo. “Maafisa wa Mali wanapenda kutoa shukurani zao kwa ECOWAS, Umoja wa Afrika, Umoja wa Ulaya, Marekani na washirika wetu wote kwa uungaji mkono wao mnamo wakati huu ambao nchi yangu inakabiliwa na mzozo mkubwa. Asanteni.”

Majeshi ya Ufaransa yaliingia nchini Mali Januari 11 mwaka huu wakati khofu ilipoongezeka kwamba wanaharakati ambao bado wanadhibiti eneo kubwa la kaskazini walikuwa wakielekea kwenye mji mkuu. Marekani imelisaidia jeshi la Ufaransa nchini Mali kwa kutoa usafiri na vifaa.
XS
SM
MD
LG