Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Machi 19, 2024 Local time: 12:46

Wakongo waomboleza kifo cha Tabu Ley


Rochereau Tabu Ley
Rochereau Tabu Ley
Mazishi ya mwanamziki Rochereau Tabu Ley aliefariki Jumamosi mjini Brussels yamepangwa kufanyika tarehe 9 Desemba. Mwili wa marehemu utasafirishwa Kinshasa Jumamosi tarehe 7.

Wakongomani wanaomboleza kifo cha Tabu Ley kwa kusikiliza muziki wake katika kila pembe ya nchi, na wimbo unaosikika sana tangu kutangazwa kifo chake ni ule anaosema "Siku nitakufa nani atanilia kwa hiyo acha ni jilie mwenyewe",

Kamati ya mazishi iliyoundwa na Meya wa Kinshasa na familia ya Rochereau wamekubalian kwamba mazishi yatafanyika Jumatatu tarehe 9 Desemba.Pascala Tabu Ley amendaliwa mazishi ya kitaifa.

Pascal Tabu Ley Rochereau kwa jina la utani Seigneur Ley, alizaliwa akiwa na jina la Pascal-Emmanuel Sinamoyi Tabu, lakini tarehe halisi ya kuzaliwa haijulikani isipokuwa inasemekana mwaka 1937 au 1940, inategemea unazungumza na nani.
please wait

No media source currently available

0:00 0:03:50 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Tabu Ley anajulikana kama muasisi wa muziki wa mtindo wa Rumba uliofahamika sana kama Soukous, alijulikana pia kwa jina la "Mfalme wa Rumba la Congo" Muziki wake unaopatikana katika mamia ya santuri za LP , umeweza kukusanywa hivi sasa na kurikodiwa kwenye CD. Muziki huo wake uliwavutia zaidi wanawake.

Tshika mkazi wa mtaa wa Limitee, Kinshasa anasema "Sote tunahusuni lakini cha kufahamu ni kwamba msani hafi kamwe. Tuna kumbukumbu ya Rochereau Tabu Ley hasa kutokana na muziki wake ulotuvutia sana. Alijenga maisha za watu na hata ndoa kutokana na muziki wake".

'Congo Avenir', wimbo wake wa mwisho na uliopata umaarufu sana, ulikuwa wa uzalendo,ambao aliimba ilikuomba wakongomani waungane pamoja kwa ajili ya kunusuru taifa lao :

Na katika tukio la nadra ,mnamo miaka ya thamanini mahasimu na majogoo wawili wa muziki wa Rumba Rochereau Tabu Ley na Luambo Makiadi, walishirikiana na kuimba wimbo uliopendwa na wengi na waliotia wenyewe "Lisanga ya banganga" yaani Ushirikiano wa Wataalamu:
I
Rochereau Tabu Ley aliyefariki akiwa na umri wa miaka 73, baada ya kuugua kiharusi tangu 2008, anatokea jimbo la Bandundu kusini magharibi mwa Kongo Tabu Ley alipata umaarufu kuanzia miaka ya sitini akiwa mwanamziki wa kwanza wa Kiafrika kuimba kwenye Jumba kuu la tamasha la Olympia la Paris Ufaransa mwaka wa 1970.
XS
SM
MD
LG