Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 15:57

Wagombea wakuu wa kiti cha rais Kenya



Uhuru Kenyatta ni mwanasiasa asiyehitaji utambulisho nchini Kenya. Ana jina ambalo ni maarufu kuliko takriban majina yote katika siasa za Kenya – KENYATTA – akiwa mtoto wa rais wa kwanza wa Jamhuri ya Kenya na shujaa wa nchini hiyo marehemu Jomo Kenyatta.

Katika ukurusa wake wa kampeni katika mtandao Uhuru ameweka picha nyingi za alivyokuwa mtoto akiwa na baba yake jomo Kenyatta lakini uhuru kwa hakika alichelewa kuingia katika siasa.
Uhuru Kenyatta (Kushoto) na mgombea mwenza wake William Ruto
Uhuru Kenyatta (Kushoto) na mgombea mwenza wake William Ruto

Baada ya kumaliza masomo katika chuo kikuu cha Amherst hapa marekani uhuru alijiingiza katika maswala ya biashara nchini Kenya kwa miaka mingi.

Haikuwa hadi mwaka 1991 ndipo uhuru alipoanza kuchomoza kichwa chake katika siasa akiunga mkono ugombea urais wa Kenneth matiba mwaka 1992 bila mafanikio na yeye mwenyewe akagombea kiti cha ubunge wa gatundu south mwaka 1997 bila mafanikio.
Wasifu wa Uhuru Kenyatta
please wait

No media source currently available

0:00 0:02:31 0:00
Kiungo cha moja kwa moja


Mwaka huu uhuru Kenyatta amekaa mahali pazuri katika ndoto yake ya kuwa kiongozi wa Kenya kama alivyokuwa baba yake. Ushirika wake wa Jubilee unamjumuisha mwanasiasa mwingine mashuhuri William Ruto hali ambayo inampa imani kubwa Kenyatta.

Hii si mara ya kwanza kwa Kenyatta kugombaia urais hata hivyo. Mwaka 2002 aliingia katika kinyang’anyiro kwa ticket ya chama cha KANU dhidi ya ushirika wa NARC uliokuwa na mwai kibaki na Raila Odinga – Kenyatta alingushwa vibaaya.

Lakini wakati huo alikuwa amekwishaingia bungeni kama mbunge wa kuteuliwa na katika uchaguzi wa mwaka 2007 aklimwunga mkono rais mwai kibaki wakati anapambana na raila odinga wa ODM

Machafuko yaliyotokea baada ya uchaguzi wa 2007 yalimtia Kenyatta katika mashitaka ambayo yanamkabili katika mahakama ya ICC huko the hague.

Akijibu swali katika mdahalo wa urais hivi karibu mjini Nairobi, Uhuru Kenyatta alisema, “katika swala la makosa ambayo tunashutumiwa nayo, hatujakutwa na hatia yoyote hii ni kesi inayoendelea na mimi na mgombea mwenza wangu tumesema waziwazi kuwa tuna nia ya kufuata utaratibu wote na kuhakikisha tunasafisha majina yetu.”

Katika kampeni ya mwaka huu Kenyatta hataji jina la baba yake, akijaribu zaidi kufanya kampeni inayoendeshwa na maswala yaliyo muhimu kwa wananchi wa Kenya – kulingana na mtizamo wake.

Katika ugombea wake mwaka huu anaongozana na William Ruto kama mgombea mwenza. Uhuru Kenyatta ana umri wa miaka 51

Raila Odinga na mgombea mwenza wake Kalonzo Musyoka
Raila Odinga na mgombea mwenza wake Kalonzo Musyoka
Raila Odinga ni miongoni mwa wanasiasa maarufu sana nchini Kenya na ambao wamekuwa katika siasa za nchi hiyo kwa miaka mingi. Ana umaarufu wa jina na ameshika nafasi mbali mbali katika serikali ya Kenya.

Kwa wengi raila odinga anaonekana kuwa mtu ambaye amekuwa akigombania urais maisha yake yote. Lakini kwa hakika hakuna maoni yanayokubaliana katika kumwelezea mwanasiasa huyo – kuna wanaomwona kuwa mtu anayesukumwa na kiu kikubwa cha kuwa rais, na wengine wanamwona kuwa mwanasiasa hodari aliyefanikiwa kudumu katika siasa za Kenya kwa muda wote huu.

Marafiki na hata wapinzani wake wanaweza kukwambia kuwa raila odinga ni mwanasiasa ambaye kwa miaka kadha sasa amekuwa moto unaoendesha mashine ya siasa za Kenya. Aliwahi kuwa mbele kuongoza juhudi za upinzani na katika kipindi cha miaka mitano iliyopita amekuwa akiongoza siasa za nchi hiyo kama waziri mkuu.

Mwaka huu raila odinga anaonekana kuwa katika nafasi nzuri sana kufanikisha ndoto yake ya kuwa rais wa Kenya.

Katika historia yake ndefu kwenye siasa za Kenya raila odinga amekuwa katika vyamba mbali mbali vya kisiasa wakati huu wote akitafuta mkusanyiko bora, unaofaa, unaokubalika, unaoweza kumfikisha katika ndoto yake ya kuwa rais wa Kenya.

Mwaka huu, kwa mara nyingine tena, anadhani amepata ushirika ulio bora – ushirika wa CORD - Coaltion for reforms and democracy – ambao utamwingiza ikulu.
Ingawa amejijengea jina lake mwenyewe katika siasa za Kenya RAILA amesaidiwa pia na jina lake la mwisho ODINGA. Baba yake, Jaramogi Oginga Odinga, alikuwa miongoni wa wapigania uhuru wa kwanza wa uhuru Kenya na aliwahi kuwa makamu rais baada ya uhuru.

Muda mfupi baada ya uhuru jaramogi Odinga aliwachia nafasi ya makamu rais baada ya kutofautiana na rais wa wakati ule jomo Kenyatta na kuanza kuongoza harakati za siasa za upinzani nchini Kenya.

Raila odinga alifuata nyayo za kisiasa za baba yake na mwaka 1982 alishutumiwa kwa jaribio la kuipindua serikali ya rais Daniel arap moi na kushikiliwa kizuizini kwa miaka sita.

Lakini alirejea nchini miaka miwili tu baadaye. Alijiunga na vyama mbali mbali na hadi hatimaye.

Hii itakuwa mara ya tatu kwa raila odinga kugombani urais na katika majaribio yake yote hayo huenda huu ni mwaka ambapo ama apate la sivyo itakuwa mwisho mwa fursa yake kuwa rais wa Kenya. Raila odinga anaumri wa miaka 68
XS
SM
MD
LG