Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 10:43

Waganda wanapiga kura Alhamis


Wananchi wa Uganda katika dakika za mwisho za kampeni.
Wananchi wa Uganda katika dakika za mwisho za kampeni.

Raia wa Uganda wanajiandaa kupiga kura Alhamis katika uchaguzi wa urais uliokuwa na kampeni zenye ushindani mkali kati ya Rais aliyeko madarakani Yoweri Museveni wa chama tawala cha National Resistance Movement-NRM na wagombea kutoka vyama vikuu vya upinzani, Dr. Kiiza Besigye wa chama cha Forum for democratic Change-FDC na Amama Mbabazi mgombea huru wa harakati za Go Forward.

Sauti ya Amerika-VOA imezungumza na mwandishi wake aliyeko mjini Kampala, Uganda anayeanza kuelezea waangalizi wa kimataifa waliopo huko wanatoka katika nchi zipi.

please wait

No media source currently available

0:00 0:02:47 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Wapigakura wataamua Alhamis kama watampigia kura Rais Yoweri Museveni aendelee kuwepo madarakani kwa muhula wa tano au kumchagua kiongozi wa upinzani na kuwa na kiongozi mpya kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1986. Rais Museveni alichukua madaraka katika mapinduzi na alishinda kwa kishindo kwenye uchaguzi wa mwaka 2006 na 2011 ambao waangalizi walisema uligubikwa na kasoro na unyanyasaji wa vyama vya upinzani.

XS
SM
MD
LG