Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 13:32

Wafaransa wengi wataka majeshi ya nchi yao kuondoka Afrika ya Kati


Wanajeshi wa Ufaransa wakifanya ukaguzi katika kituo cha ukaguzi mjini Bangui
Wanajeshi wa Ufaransa wakifanya ukaguzi katika kituo cha ukaguzi mjini Bangui
Wananchi wengi wa Ufaransa wanaitaka serikali ya nchi yao kuwarudisha nyumbani wanajeshi 1 600 walopelekwa Jamhuri ya Afrika ya Kati kujaribu kudmisha amani, na kuwapokonya silaha wapiganaji wa makundi mbali mbali.

Kufuatana na uchunguzi wa maoni ulochapishwa Jumamosi na taasisi ya IFOP, asili mia 41 tu ya wafaransa wanaounga mkono mpango wa serikali kuwaweka wanajeshi wa Ufaransa huko Jamhuri ya Afrika ya kati, kulingana na asili mia moja 51 walounga mkono mpango huo mwezi mmoja uliyopita.

Mohamed Swaleh, mchambuzi wa masuala ya kisiasa
Mohamed Swaleh, mchambuzi wa masuala ya kisiasa


Mchambuzi wa masuala ya kisiasa mjini Paris Mohamed Swaleh anasema "inavyonekana Wafaransa hawaoni faida ya wanajeshi wa nchi yao kubaki nchini humo, kwa vile hakuna adui mmoja wanaopambana nae, na ni vita vya wenyewe kwa wenyewe. Zaidi ya Hayo hawajui mapigano yataendelea kwa muda gani kutokana na hali kwamba mapambano yameongezeka".

please wait

No media source currently available

0:00 0:05:31 0:00
Kiungo cha moja kwa moja


Kwa upande mwengine uchunguzi huo wa maoni unaonesha Wafaransa wanaendelea kuunga mkono juhudi za jeshi la Ufaransa huko Mali kutokana na ushindi walopata kuwafurusha waasi wanaoungwa mkono na Al-Qaida, na kurudisha amani na umoja wa nchi hiyo.

Kufuatana na Umoja wa Mataifa zaidi ya watu 900 000 wamekimbia makazi yao tangu mapigano kuanza kati ya wanamgambo wa kikristo na waislamu wa kundi la Seleka lililompindua Rais Francois Bozize mwezi wa April mwaka 2013.

Umoja wa Mataifa unaeleza kwamba mambo yanazidi kuwa mabaya na hadi hivi sasa idara mbali mbali za umoja huo zimewafikia watu elfu 23 pekee yake kuweza kuwapatia msaada.
XS
SM
MD
LG