Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 18:49

Wafanyakazi wa umma Afrika Kusini waanza mgomo


Maelfu waliandamana mbele ya majengo ya bunge Cape Town mwanzoni mwa mwezi huu kudai mishahara wiki iliyopita.
Maelfu waliandamana mbele ya majengo ya bunge Cape Town mwanzoni mwa mwezi huu kudai mishahara wiki iliyopita.

Wafanyakazi wa huduma za umma Afrika Kusini wameanza mgomo Jumatano baada ya serikali kugoma kuwaongezea mshahara.

Wafanyakazi wa huduma za umma Afrika Kusini wameanza mgomo Jumatano baada ya kugomea nyongeza ya mshahara iliyotolewa na serikali kwa sababu ilikuwa pungufu na ile waliyotaka.

Muungano wa vyama vya wafanyakazi unaowakilisha karibu wafanyakazi millioni 1.3, ikiwa ni pamoja na waalimu, wafanyakazi wa afya, polisi na wafanyakazi wengine wa umma, wanasema wataendelea na mgomo huo mpaka madai yao yatimizwe.

Serikali imekubali kuongeza mshahara kwa asilimia 7 na imesema itaongeza marupurupu ya nyumba kutoka dolla 87 mpaka dolla 95 kwa mwezi.

Afisa wa ngazi ya juu wa serikali aliliambia bunge la Afrika Kusini juhudi zinafanywa kupata makubaliano yatakayositisha mgomo huo.

Waalimu wanasema mgomo huo utakuwa na athari zaidi kwa wanafunzi ambao tayari walikosa wiki mbili za mafunzo Afrika Kusini ilipokuwa mwenyeji wa fainali za Kombe la Dunia.

XS
SM
MD
LG