Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 14:11

Waathiriwa wa kimbunga wapata misaada


Marekani yagawa misaada kwa waathiriwa wa Philippines.
Marekani yagawa misaada kwa waathiriwa wa Philippines.
Misaada ya jamii ya kimataifa imeanza kufikia waathiriwa wa maeneo ya mbali ya Philippines, siku 10 baada ya eneo hilo kukumbwa na kimbunga kikali kwa jina Haiyan. Helikopta za Marekani zilipeleka chakula, maji na bidhaa nyingine kwa wanavijiji wa kisiwa cha Leyte na maeneo ya ndani ya nchi hiyo Jumatatu.

Marekani mpaka sasa imetoa tani 11 za msaada kuwafikia waathiriwa elfu 8. Wizara ya Ulinzi ya Marekani inasema wanajeshi 1,200 wa Marekani pia wamo nchini humo kutoa msaada.

Ndege kubwa ya mizigo USS George Washington inatumika kama kituo cha kugawa misaada hiyo ambapo helikopta zinapakia misaada na kuipeleka kwa waathirwa.

Ofisi ya mratibu wa shughuli za kibinadamu ya Umoja wa Mataifa, inasema wafanyakazi wa kutoa misaada wamepiga hatua na kuwafikia waathiriwa wengi.

Akizungumza mjini Manila, msemaji wa ofisi hiyo ya Umoja wa Mataifa Orla Fagan alisema watu kati ya milioni 8 -12 wanahitaji msaada kutokana na kimbunga hicho kilichogonga nchi hiyo Novemba 8.
XS
SM
MD
LG