Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 07:02

Waasi wa LRA waongeza visa vya ukatili nchini C.A.R


Joseph Kony (L) kiongozi wa kundi la Lord's Resistance Army na msaidizi wake Vincent Otti,
Joseph Kony (L) kiongozi wa kundi la Lord's Resistance Army na msaidizi wake Vincent Otti,

Ripoti mpya iliyochapishwa na mashirika matatu yasiyo ya kiserikali kuhusu waasi wa kundi la Lords Resistance Army- LRA inaeleza kwamba waasi hao wameendelea kuwateka nyara raia ikiwa ni juhudi za kujiimarisha kivita licha ya kushambuliwa na wanajeshi wa Uganda kwa usaidizi wa kijasusi kutoka kwa serikali ya Marekani.

Ripoti ya mashirika ya Invisible Children, The Resolve na lile la Anchor zinaeleza kwamba kundi la LRA linapata msaada wa kifedha kuendeleza mashambulizi yake kwa kuuza pembe za ndovu nchini Sudan, madini ya dhahabu pamoja na almasi katika Jamhuri ya Afrika ya kati-CAR.

Joseph Kony
Joseph Kony

Ripoti za mashirika hayo zinaongeza kusema kuwa visa vya utekaji nyara vinavyofanywa na kundi hilo hasa katika Jamhuri ya Afrika ya kati vimeongezeka kwa asilimia 32 huku mashambulizi yakiongezeka kwa asilimia 10. Licha ya jeshi la Uganda kuendelea kulishambulia kundi la waasi la LRA linalomtii kiongozi wao Joseph Kony katika msitu wa Garamba huko Jamhuri ya Afrika ya kati.

XS
SM
MD
LG