Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 16:13

Waasi wa Libya wakaribia kuingia Tripoli


Mji wa Tripoli unavyoonekana katika picha
Mji wa Tripoli unavyoonekana katika picha

Waasi wanasema wamechukua udhibiti jumamosi wa miji miwili muhimu huko zawiya upande wa magharibi na Brega iliyo mashariki mwa Libya.


Waasi wa Libya wanaosonga mbele kuingia Tripoli wamesema wamepigana mpaka karibu kilomita 30 kutoka ngome kuu ya kiongozi wa muda mrefu Moammar Gadhafi , wakati waasi katika mji mkuu wanasema wanadhibiti wilaya tatu baada ya mashambulizi yaliyoratibiwa na majeshi ya NATO .

Waasi waliosonga mbele kutokea mji wa zawiya , magharibi mwa Tripoli, wanasema majeshi ya bwana Gadhafi yalishambulia maeneo yao na roketi na mashambulizi ya anga jumapili.

Waasi wanasema wamechukua udhibiti jumamosi wa miji miwili muhimu huko zawiya upande wa magharibi na Brega iliyo mashariki mwa Libya.

Milipuko na mashambulizi mfululizo ya risasi yalisikika usiku kucha wa kuamkia jumapili katika mji wa Tripoli wakati waasi wakiushambulia mji huo.

Afisa mmoja wa baraza la taifa la mpito huko Benghazi alisema jumapili kwamba waasi walipigana katika mji wa Tripoli na wanakaribia katika makao makuu ya bwana Gadhafi lakini hakukua na thibitisho kuhusu hilo.

XS
SM
MD
LG