Wachunguzi wa Umoja wa Mataifa wanasema kampeni ya kupangwa ya ubakaji, utumwa na mauaji inayofanywa na kundi la wanamgambo wa Islamic State dhidi ya 'Yazidis' inafikia kiwango cha mauaji ya halaiki, uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu.
Tume ya uchunguzi ya Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Syria imetoa ripoti yake mapema leo ikieleza kwa kina kampeni ya makusudi ya Islamic State ya kutokomeza wakazi wa Ki-Yazidi wanaopatikana katika wilaya ya Sinjar, nchini Iraq pekee yake.
Kamishna Paulo Pinheiro amesema "mauaji ya halaiki yametokea na yanaendelea na Islamic State inahusika katika kila kukamatwa kwa wanawake, watoto ama wanaume wa Yazidi ambaye wamekamatwa na kufanyiwa ukatili mkubwa."