Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 07:41

Viongozi waahidi kuisaidia Somalia kupambana na ugaidi

Viongozi walohudhuria mkutano juu ya Somalia ulofanyika kwenye jumba la Lancaster House, London, Feb. 23, 2012.
Viongozi walohudhuria mkutano juu ya Somalia ulofanyika kwenye jumba la Lancaster House, London, Feb. 23, 2012.

Viongozi kutoka zaidi ya mataifa 50 wamewataka viongozi wa Somalia kuongoza juhudi za mageuzi ya kisiasa na kuunda serikali iliyothabiti.

Viongozi hao wamesisitiza kwamba mchakato wote wa kisiasa wa Somalia unabidi uwongozwe na Wasomali wenyewe na kusaidiwa na Jumuia ya Kimataifa.

Akiufungua mkutano huo wa siku moja mjini London siku ya Alhamisi, Waziri Mkuu wa Uingereza Davuid Cameron alisema, lengo la mkutano si kuweka vikwazo vya kimataifa dhidi ya Somalia, lakini alionya kwamba watalipa gharama kubwa ikiwa hawataisaidia nchi hiyo kujikomboa kutoka miaka mingi ya vita, ukame na umaskini.

Viongozi waahidi kuisaidia Somalia kupambana na ugaidi
Viongozi waahidi kuisaidia Somalia kupambana na ugaidi

Akizungumza na sauti ya Amerika baada ya mkutano huo mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Somalia Balozi Augustine Mahiga alisema mkutano ulikua wa kipekee kutokana na idadi ya viongozi walohudhuria na kuwepo na viongozi kutoka majimbo yote ya Somalia.

XS
SM
MD
LG