Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 26, 2024 Local time: 00:15

Viongozi wa FDLR washitakiwa


Mwanamgambo wa FDLR akiwa eneo la Goma , Drc.
Mwanamgambo wa FDLR akiwa eneo la Goma , Drc.

Kesi hiyo ya kiongozi wa FDLR Ignace Murwanashyaka na msaidizi wake Straton Musoni ilianza mei 4 mwaka 2011 kusini mwa mji wa Sturrgart nchini Ujerumani.

Mahakama nchini ujerumani Jumatatu itafanya maamuzi ya kesi moja ya muda mrefu dhidi ya viongozi wawili wa chama cha FDLR cha Rwanda kinachoshutumiwa kupanga mauaji ya halaiki mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo.

Kesi hiyo ya kiongozi wa FDLR Ignace Murwanashyaka na msaidizi wake Straton Musoni ilianza mei 4 mwaka 2011 kusini mwa mji wa Sturrgart nchini Ujerumani.

Mwaka 2009 viongozi hao wawili walikamatwa kwa kibali maalumu kilichotolewa na waendesha mashataka wa serikali ya Ujerumani ambao walithibitisha kwamba watoro hao walikuwa ni viongozi wa kundi linalosadikiwa kuwa la kigaidi la FDLR.

Kundi hilo linashutumiwa dhidi ya uhalifu dhidi ya binadamu na uhalifu wa vita dhidi ya raia nchini Congo.

Mwanzoni mwa kesi hiyo ambayo ilifanikiwa kutokana na kuhamasishwa na Umoja wa mataifa viongozi hao waliokuwa wanaishi Ujerumani kwa zaidi ya miaka 20 walishutumiwa kwa makosa 26 ya uhalifu dhidi ya binadamu na makossa mengine 39 ya uhalifu wa vita yaliyofanywa na wanamgambo chini ya usimamizi wao kati ya mwezi Januari na kukamatwa kwao mwaka 2009 huko Ujerumani mwezi novemba.

XS
SM
MD
LG