Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 03:05

Viongozi wa AU washindwa kumchagua mwenyekiti mpya


Viongozi wa AU washindwa kumchagua mwenyekiti mpya
Viongozi wa AU washindwa kumchagua mwenyekiti mpya

Viongozi wa Umoja wa Afrika wameshindwa kumchagua mwenyekiti mpya wa kamisheni ya Umoja wa Afrika, wakati wa mkutano wao huko Addis Ababa, siku ya Jumatatu.

Uchaguzi huo uliofanyika katika mji mkuu wa Ethiopia ulikua kati ya mwenyekiti wa sasa, Jean Ping kutoka Gabon na waziri wa mambo ya ndani wa Afrika kusini, Nkosazana Dlamini-Zuma.

Utaratibu ulikwama baada ya kutopatikana mshindi katika duru ya tatu ya upigaji kura, hiyo ni kutokana na kwamba hakuna mgombea yeyote aliyepeta theluthi mbili ya kura zilizohitajika kuweza kuwa mshindi.

Naibu mwenyekiti wa kamisheni ya Umoja wa Afrika-AU, Erastus Mwencha kutoka Kenya, atahudumu kama mwenyekiti wa umoja huo hadi uchaguzi mpya utakapofanyika mwezi June. Kamisheni hiyo ni chombo kikuu cha utawala cha cha AU kinachoshughulika na masuala ya biashara, usalama na masuala mengine ya sera.

Viongozi walianza mkutano wao Jumapili kwa kumchaguz Rais wa Benin, Thomas Yayi Boni, kuwa mwenyekiti mpya wa AU kwa mwaka mmoja.

Mzozo juu ya mafuta kati ya Sudan na taifa jipya la Sudan Kusini, pamoja na mzozo wa Somalia iliyoharibiwa na vita ni masuala muhimu yanayojadiliwa katika mkutano huo wa siku mbili.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, alionya Jumapili kuwa mzozo kati Sudan na Sudan Kusini umefikia “hatua mbaya” na kuwa kitisho cha amani na usalama kwa kanda zima.

Pia alielezea wasiwasi kuhusu kuongezeka kwa mzozo wa kibinadamu kwenye mpaka kati ya nchi hizi mbili.

Sudan Kusini imetekeleza kitisho chake cha uzalishaji mafuta. Nchi hiyo inadhibiti zaidi ya asilimia 70 ya mafuta katika nchi hizo mbili lakini inahitaji mabomba ya mafuta yanayopita Sudan kupeleka mafuta bandarini.

Viongozi wa nchi zote mbili walifanya mazungumzo huko Addis Ababa mwishoni mwa wiki iliyopita ili kufanya kazi pamoja kufikia makubaliano ya kugawanya mapato ya mafuta. Lakini mazungumzo yalikwama wakati Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir, aliposema hakubaliani na masharti ya gharama za usafiri..

Kusini inadai kuwa serikali ya Khartoum imezuia kinyume cha sheria mafuta yenye thamani ya mamilioni ya dola.

XS
SM
MD
LG