Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 02:08

Viongozi 150 wahudhuria mkutano wa UN


Baraza kuu la umoja wa mataifa
Baraza kuu la umoja wa mataifa

Viongozi wa mataifa makuu akiwemo rais Barack Obama, wa marekani, Xi Jinping wa China Vladimir Putin wa Russia anaehudhiuria mkutano huu kwa mara ya kwanza baada ya miaka 10, kansela wa ujerumani Angela Merkel na rais wa Ufaransa Francois Hollande Wapo mjini New York

Mkutano wa 70 wa baraza kuu la Umoja wa mataifa umeanza rasmi Jumatatu pale viongozi kutoka mataifa 150 wanapotoa hutuba zao mbele ya baraza hilo juu ya hali ya kisiasa kiuchumi na kijamii duniani.

Mkutano huu unachukuliwa kua ndio mkusanyiko mkubwa wa viongozi wa dunia, na mwaka huu ni maalum kutokana na masuala tete yaliyojitokeza kuanzia hali ya wahamiaji, vita katika pembe mbali mbali za dunia, wasi wasi wa kiuchumi, na mabadiliko ya hali ya hewa.

Viongozi wa mataifa makuu akiwemo rais Barack Obama, wa marekani, Xi Jinping wa China Vladimir Putin wa Russia anaehudhiuria mkutano huu kwa mara ya kwanza baada ya miaka 10, kansela wa ujerumani Angela Merkel na rais wa Ufaransa Francois Hollande Wapo mjini New York.

Viongozi hao wote wanatarajiwa kuzingatia juu ya vita vya Syria na athari zake hasa wakimbizi. Suala la mkataba wa nyuklia wa Iran utamulikwa wakati rais Hassan Ouhani atakapo hutubia mkutano.

Jumapili katika mkutano juu ya malengo ya milenia Rais Barak Obama ametoa wito kwa mataifa ya dunia kushirikiana kuweza kuletaa maendeleo chini ya malengo mapya ya maendeleo endelevu. Wakati huo huo alitangaza kwamba Marekani itaongeza dola milioni 300 kusaidia katika kupambana na Hiv na ukimwi.

Katika mkutano juu ya kutokomeza ukimwi uliotayarishwa na Kenya na Malawi, rais Uhuru Kenyatta alitoa wito wa ushirikiano mkubwa wa jumuia ya kimataifa ili kutokomeza uambukizaji wa HIV ifikapo mwaka 2030.

XS
SM
MD
LG