Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 23:06

Uchaguzi wa awali Marekani waingia 'Super Tuesday'


Donald Trump akizungumza katika kampeni Georgia Feb. 29, 2016.
Donald Trump akizungumza katika kampeni Georgia Feb. 29, 2016.

Mbio za kuelekea uchaguzi wa rais Marekani baadaye mwaka huu zimeingia katika moja ya siku yake muhimu kabisa Jumanne March 1 wakati wanaowania uteuzi wa vyama vyao wakipambana katika uchaguzi wa awali katika majimbo zaidi ya 10.

Wagombea ambao wamekuwa wakilegelega katika hatua za mwanzo za uchaguzi wa awali wanachukulia siku hii kama siku itakayoamua kama wataendelea na kinyang'anyiro hicho ama la.

Jumanne hii ni muhimu sana wa Mrepublican Donald Trump ambaye ameshinda majimbo matatu mfululizo na anatazamiwa kushinda katika majimbo mengine 10 katika siku hii inayojulikana kama 'Super Tuesday.' Trump yuko nyuma katika jimbo moja tu la Texas ambako ndio anakotokea mpinzani wake Seneta Ted Cruz.

Ufunguo katika mpambano wa warepublican si kwamba Trump anaweza kushinda majimbo mangapi, ila je Cruz na mgombea mwingine Seneta Marco Rubio watafanyaje kwa vile wanahitaji wajumbe wa kutosha kuweza kumpita Trump.

Hillary Clinton
Hillary Clinton

Katika kinyang'anyiro cha wademocrat, utafiti uliofanywa na makampuni ya CNN/ORC unaonyesha kuwa waziri wa zamani wa mambo ya nje Hillary Clinton anaongeza kasi yake kitaifa dhidi ya mpinzani wake Bernie Sanders kwa asilimia 55 kwa 38.

Clinton alipata ushindi wa kishindo katika uchaguzi wa awali wa jimbo la South Carolina, ushindi ambapo umemwongezea kasi baada ya kuwa ameshinda katika jimbo la Nevada kabla ya hapo.

XS
SM
MD
LG