Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Machi 19, 2024 Local time: 08:53

Wanariadha kutoka Kenya kwenye Timu ya Marekani ya Olimpiki


Wanariadha wa jeshi la Marekani Shadrack Kipchirchir na Paul Chelimo washindana kwenye mbio za majaribio ya kuchagua timu ya Olimpiki 2016.
Wanariadha wa jeshi la Marekani Shadrack Kipchirchir na Paul Chelimo washindana kwenye mbio za majaribio ya kuchagua timu ya Olimpiki 2016.

Miongoni mwa wanariadha wanaowakilisha Marekani kwenye michezo ya Olimpiki ya Rio, Brazil ni wamarekani wapya ambao wanahudumu kwenye jeshi la Marekani. Ili kupata uraia wa Marekani, mhamiaji mwenye hati maalum maarufu 'green card' hungoja miaka 5 kabla ya kupata uraiya lakini baada ya shambulizi la septemba 11, bunge la Marekani liliidhinisha kuwa wanaouhudumu kwenye jeshi wanaweza kuomba uraiya wakati wowote.

Kutokana na hilo, wanajeshi waliozaliwa kenya Paul Chelimo, Shadrack Kipchirchir na Leonard Korir wameweza kupata uraiya wa Marekani kwa wakati ili kushiriki kwenye michezo ya Olimpiki ya mwaka huu wakiwa kwenye timu ya Marekani. Wakenya hao walioko kwenye program ya mafunzo ya kijeshi ya Marekani wote ni wa kutoka kwenye eneo la bonde la ufa nchini Kenya.

XS
SM
MD
LG