Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 07:37

Upinzani Zambia waanza mazungumzo na rais aliyeko mamlakani


Rais Edgar Lungu (R) akila kiapo cha kuongoza nchi katika uchaguzi mkuu uliopita.
Rais Edgar Lungu (R) akila kiapo cha kuongoza nchi katika uchaguzi mkuu uliopita.

Katibu mkuu wa chama kikuu cha upinzani cha Movement for Democratic Change – MMD nchini Zambia anasema chama chake kimeanza mazungumzo ya awali na rais aliyepo mamlakani Edgar Lungu na utawala wake wa Patriotic Front-PF ili kuunda ushirika kabla ya uchaguzi mkuu wa August 11.

Raphael Nakachinda pia alisema amekanusha ripoti za vyombo vya habari kwamba mzozo ndani ya chama huenda ukavuruga uwezekano wa kuunda ushirika na PF kabla ya uchaguzi wa rais, bunge na serikali za mitaa.

Alisema hatua ya kufanya mazungumzo ya awali na PF imekuja ikiwa ni matokeo ya kipengele kipya cha katiba ambacho kinasema kwamba unaweza kushinda uchaguzi kama mgombea atapata walau asilimia 51 ya kura zote zilizopigwa. Awali mgombea anaweza kutangazwa mshindi akiwa amepata chini ya asilimia 50 ya kura.

Rais Lungu hakuficha aliposema ili kuweza kufanikisha hilo inamlazimu kufanya kazi na vyama vingine vya siasa. Na MMD ni moja ya vyama vya siasa ambavyo amevitaja angependa kuunda ushirika nao, alisema Nakachinda.

XS
SM
MD
LG