Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 17:22

Upinzani Tanzania waungana kujaribu kukiondowa madarakani CCM


Wafuasi wa UKAWA wahudhuria sherehe za kutiwa saini makubaliano ya kuungana
Wafuasi wa UKAWA wahudhuria sherehe za kutiwa saini makubaliano ya kuungana

Viongozi wa vyama vinne vikuu vya Tanzania, CHADEMA, CUF, NCCR - Mageuzi na NDL, wametia saini Mkataba wa Muelewano MOU, kuungana pamoja katika juhudi za kuendesha kapmeni za pamoja kupinga rasimu ya katiba mpya pamoja na kushirikiana katika uchaguzi wa mitaa, majimbo na taifa.

Viongozi hao wanaoungana chini ya Umoja wa Katiba ya Wananchi, UKAWA, walikutana na umati mkubwa wa wafuasi wao kwenye viwanja vya Jangwani siku ya Jumapili na kukubaliana kufanya kazi pamoja.

Maalim Seif Sharif Hamad, Katibu wa chama cha Wananchi, CUF na makamu wa kwanza wa rais, alisema, "Wananchi wenzangu tuko hapa kwa tukio adhimu ya kushuhudia vyama vyetu vinaweka saini makubaliano ya kufanya kazi kwa pamoja ili kukin'gowa chama cha CCM.

Mkataba huo wenye vipengele saba, miongoni mwa mambo mengine unasisitiza kwamba vyama hivyo vinne vitashirikiana pamoja katika, kuelimisha wananchi kuifahamu na kupiga kura ya hapana dhidi ya rasimu ya katiba, kupanga utaratibu wakushirikiana katika uchaguzi wa serikali za mitaa baadae mwaka huu na uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, na kuwa na wagombea wa pamoja katika viti vyote vinavyopiganiwa.

Viongozi hao wameahidi kuungana bila ya kujali maslahi yao binafsi na kuwa na wagombea wapamoja katika uchaguzi wote.

please wait

No media source currently available

0:00 0:03:31 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Baadhi ya wachambuzi wa mambo hata hivyo, wanahoji ikiwa umoja huo utaweza kuwa na nguvu za kuhimili kishindo cha chama tawala cha CCM, ambacho wengine wanasema chama hichop katika uchaguzi mkuu uliyopita kilijipatia asili mia 60 za kura dhidi ya asili mia 40 za upinzani.

Mbaraka Islam wa Raia Mwema na Jamiifroum anasema nimapema kusema jinsi muungano huo utafanya kazi kwani ni mara ya kwanza kwa viongozi wa upinzani kutia saini makubaliano ya kushirikiana pamoja.

XS
SM
MD
LG