Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 23, 2024 Local time: 12:06

Upinzani DRC wapata pigo


Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe na Rais Joseph Kabila wa DRC
Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe na Rais Joseph Kabila wa DRC

Etienne Tshisekedi akataa mwito wa kuungana na vyama vya upinzani

Juhudi za upinzani katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo za kupata mgombea mmoja wa kiti cha urais,zimevunjika kufuatia msimamo wa Etienne Tshisekedi wa kujitangaza kuwa mgombea wa chama chake cha UDPS.

Mpinzani mwingine Vital Kamerhe ambaye amesikitishwa na hatua hiyo ya Tshisekedi amesema lengo la upinzani hivi sasa ni kumwangusha rais aliyeko madarakani hivi sasa Bw. Joseph kabila kupitia uchaguzi licha ya tofauti miongoni mwa wapinzani.

Jumatano vyama vidogo kama vinane hivi, vimemuunga mkono Etienne Tshisekedi kama mgombea wa kiti cha urais na kuunda vuguvugu jipya la kumuunga mkono.

XS
SM
MD
LG