Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 09:14

Upinzani Afrika kusini unasema ANC haina nafasi katika uchaguzi


Baadhi ya wafuasi wa upinzani nchini Afrika kusini. Julai 27, 2016.
Baadhi ya wafuasi wa upinzani nchini Afrika kusini. Julai 27, 2016.

Mwanachama mmoja wa upinzani wa Democratic Alliance cha nchini Afrika kusini alisema maneno anayotumia Rais Jacob Zuma kabla ya uchaguzi wa serikali za mitaa siku ya Jumatano ni ishara ya kuchanganyikiwa kwamba chama tawala cha African National Congress-ANC huwenda kikashindwa na upinzani katika misingi ya umaarufu.

Rais Zuma Jumapili aliwahamasisha waa-Afrika kusini kukipigia kura chama cha ANC ili chama hicho kiendelee kuboresha maisha yao. ANC inadhibiti viti vya miji 278 nchini humo lakini kura mpya za maoni zinaonesha kwamba ANC ina wakati mgumu katika miji ya Pretoria, Johannesburg na Port Elizabeth.

Sheila Camerer, balozi wa zamani wa Afrika kusini na mwanachama wa Democratic Alliance alisema wakati huu wa-Afrika kusini wengi hawatamsikiliza Rais Zuma kwa sababu wanahisi maisha yao hayajaboreka chini ya utawala wa miaka kadhaa ya ANC.

XS
SM
MD
LG