Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 01:53

Fedha zahitajika kusaidia watoto wanaokumbwa na majanga duniani


Mtoto katika mojawapo ya maeneo yaliyokumbwa na majanga duniani.
Mtoto katika mojawapo ya maeneo yaliyokumbwa na majanga duniani.

Idara ya watoto ya Umoja wa Mataifa-UNICEF inatowa wito wa kupatikana dola billioni 2.8 kwa ajili ya kulinda na kusaidia takriban watoto millioni 43 kote duniani wanaojikuta kati kati ya majanga ya kimataifa ikiwa ni pamoja na migororo, magonjwa, na mabadiliko ya hali ya hewa.

Wito wa mwaka huu wa UNICEF ni mdogo kidogo kuliko wito wa mwaka jana ambapo mlipuko wa virusi vya Ebola huko Afrika magharibi ulihitaji kiwango kikubwa cha fedha kilichotengwa kwa ajili ya hali za dharura kote duniani.

Shirika la kuhudumia watoto duniani-UNICEF
Shirika la kuhudumia watoto duniani-UNICEF

Kwa mara ya kwanza UNICEF inaeleza kiwango kikubwa cha fedha hizo takriban asilimia 25 kitatumiwa katika kuwapatia elimu watoto walioko kwenye mazingira ya dharura. Idara hiyo ilisema inapanga kutowa elimu kwa zaidi ya watoto millioni 8 mwaka huu.

Takriban watoto millioni 5 kati ya hao watakuwa watoto wa Syria waliopo ndani ya nchi au ambao ni wakimbizi katika nchi jirani.

Mwakilishi wa UNICEF nchini Syria, Hanna Singer, anajuwa ugumu wa vita kwa watoto. Anaiita Syria mahala hatari zaidi duniani kwa mtoto kuwepo.

Watoto wa Syria wakiwa ndani ya tundu huko Damascus
Watoto wa Syria wakiwa ndani ya tundu huko Damascus

Ufadhili wa wito huu wa UNICEF pia utasaidia watoto wanaoathirika kutokana na upungufu mkubwa wa chakula, ghasia, magonjwa na kunyanyaswa.

Idara hiyo ya Umoja wa Mataifa inaeleza kuwa mabadiliko ya hali ya hewa ni kitisho kinachoendelea kukuwa, kukiwa na mamillioni ya watoto wanaoishi katika maeneo ambayo yanakumbwa na mafuriko au ukame mbaya. Miradi mingine inalenga kuwasaidia watoto katika mazingira mabaya ya kisiasa kama vile Burundi na nchi zinazopakana na mto Chad.

XS
SM
MD
LG