Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 23, 2024 Local time: 17:12

UNHCR yatoa wito kwa Kenya kutofunga kambi za wakimbizi


Baadhi ya wakimbizi katika kambi ya Dadaab iliyopo Kenya.
Baadhi ya wakimbizi katika kambi ya Dadaab iliyopo Kenya.

Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa-UNHCR linatoa wito kwa nchi ya Kenya kufikiria mipango yake ya kufunga makambi mawili makubwa ya wakimbizi nchini humo likisema hatua hiyo italeta madhara makubwa kwa maelfu ya watu.

UNHCR ilisema katika taarifa yake ya Jumatatu ambayo ilitathmini mipango ya serikali ya Kenya na kuelezea wasi wasi wake. Shirika hilo limeisihi serikali kuepuka hatua yeyote ambayo inaweza ikakiuka masharti ya kimataifa na ilisema usalama wa maelfu ya wakimbizi wanategemea hisani ya kenya.

Kenya ilitangaza Ijumaa kwamba itafunga makambi ya wakimbizi ya Dadaab na Kakuma ndani ya kipindi cha muda mfupi ikieleza wasi wasi wa usalama hususani kutoka al-Shabab kundi la wanamgambo wa ki-Islam kutoka Somalia ambalo limefanya mashambulizi kadhaa makubwa nchini Kenya.

Ilisema kwamba kuendelea kuwapa hifadhi wakimbizi ambao wengi ni kutoka Somalia ni sehemu kubwa ya changamoto za usalama.

XS
SM
MD
LG