Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 01:37

UNHCR yakadiria watu 880 wamekufa wakijaribu kuvuka bahari ya Mediterranean


Wahamiaji wakiokolewa na jeshi la majini la Italy kwenye bahari ya Mediterranean.
Wahamiaji wakiokolewa na jeshi la majini la Italy kwenye bahari ya Mediterranean.

Inakadiriwa wahamiaji na wakimbizi 880 wamekufa wakati wakijaribu kuvuka bahari ya Mediterranean wiki iliyopita shirika la kuhudumia wakimbizi katika Umoja wa Mataifa-UNHCR lilitangaza Jumanne.

Idadi hiyo inajumuisha watu waliopoteza maisha katika miezi mitano ya kwanza yam waka huu na kufikia zaidi ya 2,500 ambao walijaribu kufika ulaya miongoni mwa maelfu ya watu. Ukilinganisha na watu 1855 walikufa katika kipindi hicho mwaka jana.

Taasisi za kibinadamu zimesambaza picha ya mfanyakazi mmoja wa Ujerumani akimshikilia mtoto mmoja aliyezama ili kuvuta mwamko wa dunia kutokana na tatizo hilo.

Wahamiaji wengi wanaofanya safari hizi wanatokea Nigeria na Gambia, pamoja na wa-Syria, wa-Afghanistan na wa-Irak wanaendelea kutumia njia ya Uturuki hadi Ugiriki, kwa mujibu wa UNHCR.

Waziri wa mambo ya nje wa Denmark, Kristian Jensen alisema Jumanne baada ya mkutano na mwenzake wa Hungary, Peter Szijjarto, kwamba umoja wa ulaya-EU lazima usimame pamoja kupunguza mmiminiko wa wahamiaji wanaoingia kwenye eneo hilo.

Waziri wa mambo ya nje wa Hungary, Peter Szijjarto.
Waziri wa mambo ya nje wa Hungary, Peter Szijjarto.

Szijjarto alisema tatizo la wahamiaji ni changamoto kubwa sana ambayo iliikumba umoja wa ulaya tangu kuundwa kwake. Umoja huo lazima ulinde mipaka yake au ulaya haitaweza kukabiliana na changamoto za uhamiaji, alisema. “Bila ya kulinda mipaka yetu, ulaya haiwezi kukabiliana na changamoto hili, ambayo ni kubwa sana na hatujawahi kukabiliana nayo tangu kuanzishwa kwa umoja wa ulaya. Hungary imefanya mengi ili kulinda mipaka yake. Tutaendelea na hilo, na pale itakapokuja suala la kujadili mshikamano, hatudhani mshikamano unamaanisha kuwapeleka wahamiaji kutoka mpaka mmoja wa EU kwenda mpaka mwingine. Mshikamano unamaanisha kuheshimu majukumu yenu, na kuheshimu kanuni za kimataifa na kwamba unasitisha mmiminiko wa wahamiaji haramu”.

Hungary imeweka vituo vitatu kwa ajili ya utaratibu wa wanaotafuta hifadhi baada ya kujenga uzio wa chuma kwenye mipaka yake na Serbia na Croatia ili kupunguza mmiminiko wa wahamiaji kuingia ulaya magharibi. Denmark imeongeza udhibiti kwenye mipaka yake ya kusini na Ujerumani.

XS
SM
MD
LG