Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 01:41

Umoja Mataifa yaelezea wasiwasi kuhusu hali ya raia nchini Yemen


Jengo liloharibiwa kutokana na vita huko mjini Sanaa, Yemen.
Jengo liloharibiwa kutokana na vita huko mjini Sanaa, Yemen.

Ripoti ya hivi karibuni juu ya jopo maalum kwa harakati za raia, inaonyesha kuwa zaidi ya watu millioni 2.4 sasa wamepoteza makazi yao nchini Yemen.

Idara za umoja mataifa zinaelezea ongezeko la wasiwasi juu ya mamillioni ya watu ambao wamelazimishwa kuondoka makwao kutokana na vita vinavyoendelea vya takriban mwaka mmoja nchini Yemen. Umoja mataifa unaripoti kuwa zaidi ya raia elfu 3 wameuwawa na wengine takriban elfu 6 kujeruhiwa tangu Saudi Arabia ilipoanza kuwapiga mabomu waasi wa kihouthi hapo March 26, mwaka 2015. Idadi hizo haijumuishi watu waliojeruhiwa miongoni mwa vikosi vinavyopigana

Msemaji wa masula ya wakimbizi katika Umoja Mataifa, Leo Dobbs, anasema ripoti ya hivi karibuni juu ya jopo maalum kwa harakati za raia, inaonyesha kuwa zaidi ya watu millioni 2.4 sasa wamepoteza makazi yao nchini Yemen.

Bw. Dobbs anasema, idadi hii inashtusha sana na inatia wasiwasi mkubwa, na hali huwenda ikazorota zaidi kutokana na kuongezeka kwa hali mbaya ya kibinadam iliopo huko na hali ya mbaya zakijamii na kiuchumi, na kadhalika kutokuwepo kwa suluhisho la kisiasa.

Dobbs anasema wengi walopoteza makazi wako katika maeneo 5 ambapo mzozo umekihiri zaidi nayo ni Taizz, Hajjah, Sana’a, Amran na Sa’ada.

Bw. Dobbs anasema, wamekuwa wakijaribu kupeleka misaada katika maeneo hayo, tunazisihi pande zote kuruhusu misaada ya kibinadam kufika maeneo yaloathiriwa zaidi.

Muungano unaongozwa na Saudi Arabia umeweka kizuizi kwa upelekaji chakula, dawa mafuta na bidhaa nyingine muhimu kwa takriban mwaka mmoja uliopita. Mara kwa mara, kumelegezwa vikwazo, na hivyo kuruhusu baadhi ya bidhaa za kuokowa maisha kuingia yemen, lakini havitoshi.

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM linaeleza kuwa lina wasiwasi mkubwa kuhusu hali ya maelfu ya raia wa mataifa mengine ambao wamejikuta ndani ya mzozo. Ripoti inaeleza kuwa watu hao hukumbwa na kila aina ya ghasia na vurugu.

Msemaji wa IOM Joel Millman anasema maelfu ya wasomali wanaotafuta hifadhi na wahamiaji wa kiethopia ambao hupitia mashariki ya kati, sasa wamekwamanchini Yemen ilogubikwa na vita.

Millman anasema, kuna imani kubwa kuwa takriban watu elfu 92 waliweza kuingia Yemen mwaka jana kutoka Somalia na Ethiopia. Sasa hawajulikani walipo. Anasema wanajuwa kuwa baadhi yao wameweza kufika kule walipokuwa wakielekea, lakini tunajuwa kuwa pia wengine wengi hawakufanikiwa. Kuna wasiwasi juu ya kutekwa nyara na kuzuiwa nchini yemen hivi sasa .

Umoja Mataifa umeomba takriban dola billioni 1.8 mwezi ulopita ili kutowamsaada wa kibinadam kwa watu millioni 13.6 ambao wanauhitaji. Hadi sasa ni takriba asli mia 2 tu ya fedha hizo ambazo zimeweza kupatikana.

XS
SM
MD
LG