Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 16, 2024 Local time: 19:56

UN yafungua Ofisi Mogadishu


mwakilishi maalumu wa UN nchini Somalia Augustine Mahiga, kulia akiwa na waziri mkuu wa somalia Abdiweli Mohamed Ali,
mwakilishi maalumu wa UN nchini Somalia Augustine Mahiga, kulia akiwa na waziri mkuu wa somalia Abdiweli Mohamed Ali,

tangu miaka 17 iliyopita haikuwahi kuwa na ofisi ya UN mjini Mogadishu

Umoja wa Mataifa umefungua ofisi ya kisiasa katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu, baada ya kutokuwepo na ofisi katika nchi hiyo kwa miaka 17.

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Somalia, balozi Augustine Mahiga, aliwasili kwenye uwanja wa ndege wa Mogadishu hii jumanne, na kukaribishwa na Waziri Mkuu, Abdiweli Mohamed Ali na maafisa wengine wa serikali na wanadiplomasia.

Mahiga ameelezea matumaini kwamba kufunguliwa kwa ofisi ya masuala ya kisiasa ya Umoja wa Mataifa kutaweza kurejesha matumaini mapya ya hali ya baadae nchini Somalia.

Amesema ofisi mpya itasaidia umoja huo kufanya kazi kwa karibu na serikali kuu ya mpito nchini Somalia.

XS
SM
MD
LG